Imeripotiwa kuwa Watu wanaokadiriwa kuwa sita wamevamia
nyumbani kwa Ally Faki 45 mfanyibiashara ,mvuvi, mkazi wa petukiza na kumjeruhi
kwa panga sehemu ya kichwani kisha kupora Tsh 1,200,000.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa polisi
mkoani hapa Frasser Kashai amesema tukio hilo limetokea mnamo tarehe 31 octoba mwaka huu majira ya
saa 8 usiku huko Petukiza Kijiji cha
Mwaboza Kata Ya Moa Tarafa ya Mkinga Wilaya ya Mkinga .
Aidha Kamanda Kashai amesema hali ya Majeruhi
inaendelea vizuri na ameruhusiwa kutoka hospitalini alipokuwa anatibiwa.
Sambamba na hayo Kamanda Kashai amesema hakuna
aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo na
msako mkali unaendelea ili kuwabaini waliotenda tukio hilo.
Jeshi la polisi linatoa Wito kwa wananchi kuendelea kuonyesha ushirikiano wa
kutoa taarifa za kisiri juu ya uwepo wa wahalifu katika maeneo yao wanayoishi
ili kuweza kuzuia na kukabiliana na uhalifu.
No comments:
Post a Comment