KAMANDA WA POLISI MKOA WA TANGA FRASSER
KASHAI
|
Na Redeca Duwe na Daniel Raphael.TANGA
Mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Raba Kajenje mwenye umri wa miaka 32, mvuvi
na mkazi wa kipumbwi Kata Tarafa ya
Mwera Wilayani Pangani Mkoani hapa amekutwa amekufa maji baharini
wakati anavua samaki.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani hapa Frasser Kashai amesema tukio hilo
limetokea mnamo tarehe 30 septemba mwaka
huu.
Hata hivyo
kamanda Kashai amesema kuwa chanzo cha
kifo hicho ni kushindwa kuogelea baada
ya kuanguka kwenye maji
Katika tukio kama hilo mtu mmoja
anayefahamika kwa jina la Eliza Shorori mwenye umri wa miaka 33 mkulima mkazi wa mnazi
Kata ya Daluni Tarafa ya Maramba Wilaya ya Mkinga Mkoani hapa amekutwa akiwa
amekufa maji katika mto wa Bombo kijiji cha Maramba.
Akithibithisha
kutokea kwa tukio hilo Kamanda Kashai amesema tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 30 septemba mwaka huu majira ya
saa nane mchana na chanzo cha kifo hicho ni marehemu kuwa na tatizo la kuanguka
kifafa.
KATIKA TUKIO JINGINE Zaidi ya shillingi TSH
,700,000 ikiwa ni pamoja na vitu vya thamani kama dhahabu zenye thamani
ya zaidi ya Tsh 3,000,000 zimeibiwa na watu wasiojulikana kwa kuvunja nyumba ya
Kibibi Mashaka mwenye umri wa miaka 43 mjasiria mali na mkazi wa Sahare kwa kuvunjiwa nyumba yake kwa kutumia jiwe
kubwa.
Akizungumza
nawaandishi wa habari ofisini kwake leo kamanda wa jeshi la polisi mkoana hapa
Fresser Kashai amesema tukio hilo lime tokea mnamo tarehe 01 octoba mwaka huu
majira ya saa 01:45 usiku wa kuamkia leo huko maeneo ya Sahare kata ya mzingani
wilayani Tanga mkoani hapa.
Aidha
Kashai mesema msako mkali unaendelea na hadi sasa hakuna mtu alie kamatwa
kuhusiana na tukio hilo.
Sanjari na
hayo jeshi la polisi mkoani hapa limetoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano
kwajeshili la polisi kuhakikisha wanatoa taarifa na kufichua vitendo vya
uhalifu vinavyoendelea ndani ya jamii.
No comments:
Post a Comment