Watu wenye ulemavu walipofunga Barabara Jijini Dar kudai haki zao (Picha na Maktaba) |
Na.Masanja Mabula_Pemba.
Jamii imetakiwa
kutowatenga na kuwathamini watu wenye ulemavu katika maeneo wanaoishi kwa
kuhakikisha inapawapatia haki zao za msingi ikiwemo haki ya elimu .
Mratibu wa jumuiya ya
vijana ya umoja wa mataifa pemba bw mohammed hassan ali amesema kuwa watu
wenye ulemavu wana haki sawa na watu wengine hivyo kuwatenga
kunasababisha kuzikosa haki zao stahiki .
Akizungumza na Redio Huruma
kisiwani hapa , mohammed amesema kuwa walemavu wanatakiwa kupatiwa haki zote za
msingi kama watu wengine na kwamba tabia ya baadhi ya wanajamii ya kuwatenga ni
kwenda kinyume na msingi ya haki ya binadamu .
Aidha amefahamisha
kwamba walemavu wanatakiwa kushirikishwa katika ngazi za kutoa maamuzi kwenye
jamii kwani michango yao inaweza kuleta mabadiliko chanya ya maendeleo .
Ameeleza kwamba baadhi
ya wanajamii wamekuwa wakiwatekeleza watu wenye ulemavau kutokana na maumbile
yao hali ambayo inasababisha wajiunge na makundi maovu ikiwemo ya utumiaji wa
madawa za kulevya .
Hata baadhi ya watu
wenye ulemavu wameiambia redio maria kuwa bado jamii na serikali imeshindwa
kutekeleza baadhi ya kero zinazowakabili ikiwemo suala la kuweka huduma rafiki
kataika majengo ya taasisi zake na za watu binafsi .
No comments:
Post a Comment