HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Wednesday, 22 October 2014

KUJUA KILICHOJIRI UEFA CHAMPIONS LEAGUE JANA NA KITAKACHOJIRI LEO..! click hapa



RATIBA/MATOKEO:
Jumanne Oktoba 21
KUNDI E
CSKA Moscow 2 Man City 2
AS Roma 1 Bayern Munich 7
KUNDI F
APOEL Nicosia 0 Paris St-Germain 1
Barcelona 3 Ajax 1
KUNDI G
Chelsea 6 NK Maribor 0
FC Schalke 4 Sporting Lisbon 3
KUNDI H
BATE Borisovs 0 Shakhtar Donetsk 7
FC Porto 2 Athletic Bilbao 1
Mshambuliaji wa Shaktar LUIZ ADRIANO "alifunga bao 5 kati ya 7 dhidi ya BATE Borisov jana

+++++++++++++++++++++++++++++
AS Roma 1 Bayern Munich 7
Wakicheza kwao Olimpico Stadium Jijini Rome kwenye Mechi ya Kundi E, AS Roma wameshushiwa kipigo kitakatifu na Bayern Munich kwa kutandikwa Bao 7-1.
Bayern walifunga Bao la kwanza katika Dakika ya 8 baada ya Nahodha Phlipp Lahm kumpa pasi Arjen Robben aliachia shuti hadi wavuni.
Bao nyingine za Bayern zilifungwa katika Dakika ya 23 na Mario Gotze, Dakika ya 25 na Robert Lewandowski na Arjen Robben kufanya Bayern 4 AS Roma 0 katika Dakika ya 30.
Arjen Robben
Bayern walifunga Bao lao la 5 kwenye Dakika ya 35 kwa Penati ya Thomas Muller ambayo ilitolewa kufuatia Manolas kuunawa Mpira.
Hadi Mapumziko AS Roma 0 Bayern Munich 5.
Gervinho aliipa Bao AS Roma kwenye Dakika ya 66 kufuatia ushirikiano mzuri wa Florenzi na kisha Nainggolan kutumbukiza Krosi iliyounganishwa wavuni kwa Kichwa na Gervinho.
Franck Ribery, alieingizwa badala ya Lewandowski katika Dakika ya 68, aliipa Bayern Bao la 6 Dakika ya 78 na Bao la 7 kwa Bayern kufungwa na Xherdan Shaqiri, aliembadili Mario Gotze katika Dakika ya 79, na Bao hilo liliingia Dakika ya 80.
Hadi mwisho AS Roma 1 Bayern Munich 7.
Barcelona 3 Ajax 1
Wakiongozwa na Mastaa wa Argentina na Brazil, Lionel Messi na Neymar, Barcelona wakiwa kwao Nou Camp wameichapa Ajax Bao 3-1 katika Mechi ya Kundi F.
Bao la kwanza lilipatikana katika Dakika ya 7 lilipoanzia kwa Lionel Messi aleicheza vizuri kwa kuisakama Difensi na kisha kumpa Neymar aliefunga Bao safi.
Barca walifunga Bao lao Pili Dakika ya 24 baada ya pasi ya Iniesta kumaliziwa vizuri na Lionel Messi.
Lionel Messi na Neymar
Hadi Mapumziko Barcelona 2 Ajax 0.
Kocha wa Barca, Luis Enrique, akiwa na jicho moja Jumamosi huko Santiago Bernabeu kwenye mtanange wa El Clasico dhidi ya Mahasimu wao Real Madrid, aliamua kumpumzisha Lionel Messi katika Dakika ya 66 na kumuingiza Chipukizi Mounir El Haddadi.
Chipukizi wa Miaka 19, Anwar El Ghazi, alieingizwa Dakika ya 73 kumbadili Sigthorsson, aliipa Bao Ajax katika Dakika ya 88.
Katika Dakika ya 94 Sandro Ramirez aliipa Barca Bao la 3 na kuipa ushindi wa 3-1.
Chelsea 6 NK Maribor 0
Uwanjani Stamford Bridge, Wenyeji Chelsea wameichakaza NK Marbor kwa kuichapa Bao 6-0 katika Mechi ya G.
Chelsea walifungua kitabu cha Magoli Dakika ya 13 baada ya  pasi safi ya John Terry kumfungulia njia Loic Remy aliefunga vizuri na kuipa Chelsea Bao la kuongoza.
Juhudi hiyo ya Remy ilimfanya aumie Nyonga na Dakika chache baadae kutoka nje na nafasi yake kuchukuliwa na Didier Drogba.
Drogba aliipa Chelsea Bao la Pili katika Dakika ya 22 kwa Penati iliyotolewa baada ya Pasi ya Willian kumgonga mkononi Ales Mertelj.
John Terry aliipa Chelsea Bao la 3 katika Dakika ya 30 kufuatia kaunta ataki safi iliyoanzia kwa Drogba kuokoa Mpira langoni wakati wa Kona na Eden Hazard kukokota Mpira hadi eneo la Maribor na kumpasia Cesc Fabregas aliempa Terry, aliepanda toka Difensi, na kufunga.
Nahodha wa Chelsea John Terry
Hadi Mapumziko Chelsea 3 NK Marobor 0.
Kipindi cha Pili Dakika ya 54, Chelsea walipata Bao la 4 la kujifunga wenyewe kufuatia krosi ya Eden Hazard kumgonga kwenye kisigino Mitja Viler na kutinga.
NK Maribor walipata Penati katika Dakika ya 64 iliyotolewa baada ya Nemanja Matic kumchezea Rafu Agim Ibraimi ambae alipiga mwenyewe na kugonga Posti.
Chelsea walifunga Bao la 5 kwa Penati waliyopata baada ya Marko Suler kumshika Branislav Ivanovic na kumwangusha na Penati hiyo kufungwa kifundi na Eden Hazard katika Dakika ya 77.
Dakika ya 90, Eden Hazard aliipa Chelsea Bao la 6 baada kupokea na kutuliza pasi ya juu toka kwa Nathan Ake na kumpunguza Beki mmoja na kufunga.
Hadi mwisho, Chelsea 6 NK Maribor 0.
RATIBA
**Mechi zote kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku
**Saa za Bongo
Jumatano Oktoba 22
KUNDI A
Atlético Madrid v Malmö FF
Olympiakos v Juventus
KUNDI B
Liverpool v Real Madrid
Ludogorets Razgrad v FC Basel
KUNDI C
Bayer 04 Levserkusen v Zenit St Petersburg
Monaco v Benfica
KUNDI D
Galatasaray v Borussia Dortmund
RSC Anderlecht v Arsenal

No comments:

Post a Comment