Wakulima wa Karafuu wa kianika zao hilo(Picha na Makataba) |
Baada ya kukithiri kwa
vitendo vya wizi wa karafuu kwa kukatwa matawi au mashina ya
mkarafuu , wakulima wa zao hilo Kisiwani Pemba wameitaka Serikali kuandaa
utaratibu wa kuuhifadhi na kuulinda mkarafuu ili uendelee kuwa tegemeo la
Uchumi wa Taifa .
Wamesema kuwa iwapo
Serikali haitajaweka utaratibu wa kuulinda na kuuhifadhi mkarafuu upo uwezekano
wa zao hilo kupoteza hadhi kwani wizi wamekuwa wakiikata mikarafuu na kisha
kwenda kuchambulia sehemu nyingine na kisha karafuu kuziuza kwa
wafanyabiashara wa magendo kwa njia ya vikombe na pishi .
Baadhi ya wakulima wa
karafuu wamesema kuwa kutokana na kukithiri kwa vitendo hivyo na wahusika
wanaowakamata kushindwa kuchukuliwa hatua na vyombo vya Sheria , hali hiyo
inaweza kusababisha wajichukulie sheria mikononi mwao .
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar
Khamis Othman akizungumzia tatizo hilo amewataka wakulima kuondoa rushwa muhali
wakati wanapo wakamata watu wakiwa wanafanya hujuma kwenye mashsmba ya
mikarafuu ili waweze kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria .
Hata hivyo Mkuu huyo wa Mkoa
amewtaka wakulima kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika
kufanikisha ulinzi na uhifadhi wa mkarafuu na karafuu kwani mkarafuu ukikatwa
mkulima hawezi kupata karafuu.
No comments:
Post a Comment