Na Masanja Mabula PEMBA
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe
Omar Khamis Othman amewataka wakuu wa Idara za Serikali na binafsi kutoa fursa
kwa wafanyakazi wao kujiendeleza kielimu ili waweze kukabiliana na changamoto
za mabadiliko ya Kilelimu zinazojitokeza siku hadi siku.
Amesema kuwa kila Mkuu wa Idara za
Serikali na binafsi anapaswa kuhakikisha wafanyakazi wake wanajiendeleza
kielimu ili kukidhi matakwa ya urandawazi .
Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza
kwenye kilele cha Shereha za maadhimisho ya juma la Elimu ya watu wazima
ambapo kwa Pemba zilizofanyika katika viwanja vya Skuli ya
Shengejuu Wilaya ya Wete.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa ametoa wito kwa
vijana walioshindwa kuendelea na masomo ya kidato cha tatu na nne katika skuli
za Serikali kujiunga na vituo vya kujiendeleza vilivyo katika mikoa ya Pemba .
Mhe Omar amewahimiza msheha
kushirikiana na walimu wakuu kuorodhesha vijana walioacha Skuli ili wafunguliwe
madarasa ya Elimu Mbadala katika shehia zisizo na madarasa ya kisomo .
Kwa upande wake Mtatibu wa
Elimu ya Mbadala na watu wazima Pemba Mwalim Hija hamad Issa amesema kuwa lengo
la Idara hiyo ni kuhakikisha kuwa vijana wote waliokosa elimu ya lazima
wanajiunga na madarasa ya kisomo cha watu wazima .
No comments:
Post a Comment