Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Omar Guledi(Picha na Maktaba) |
Na
Rebeca Duwe. TANGA
Baadhi ya
wafanya biashara wa soko la mlango wa chuma liliopo maneo ya barabara
kumi na tano mkoani hapa wameilalamikia Manispaa ya
jiji la Tanga kwa madai ya kuchukuliwa bidhaa
zao na Mgambo. bidhaa ambazo wanauza kwa ajili ya kujipatia kipato.
Wakizungumza na redio huruma wafanyabiashara hao
wamesema kuwa bidhaa zao zimechukuliwa bila kufuatwa utaratibu kwani utaratibu uliokwepo ni kwamba
wanaofanya biashara ya jumla wanatakiwa kuwepo maeneo hayoa kuanzia saa kumi na
moja mpaka saa nne abuhi ndipo utaratibu
mwingine ufuatwe na badala yake wameshtukiziwa bado hata wengine hawajaanza
kuuza.
Kwa upande wake katibu wa Soko hilo Bw. Kimweri Zayumba
amekiri wafanya biasahra hao kuchukuliwa bidhaa na hatimaye kurudi majumbani
mwao blia faida na kusema kuwa Manispaa hawana makosa bali wamefanya hivyo
kutokana na wafanya baishara hao kuuzia bidhaa zao maeneo ya barabarani ambapoa
ni kinyume na utaratibu wa kufanya biashara.
Aidha ametaja changamoto katika soko hilo kuwa ni
ukarabati wa maeneo ya soko na ujenzi wa
kuta za soko hilo pamoja na kuboresha mandhari ya soko kwani walisha toa barua ya
kuomba ukarabati lakini bado hawajapata majibu.
Hata hivyo Afisa masoko na biashara jiji la Tanga
bw.Raslidi Gogola amesema manispaa
wamefanya hivyo kwa utarabu uliowekwa kwani maeneo ya barabara hayaruhusiwi kufanyia biashara yeyote .
Lakini pia Afisa huyo amesema kutokana na madai yao ya
kuboreshewa mazingira pamoja na ukarabati manispaa imejipanga vizuri kwani sasa file lao liko kwa mhandisi
wa jiji la Tanga ambapo mara baada ya kukamilika halmashauri itamtafuta
Mzabuni kwa ajili ya kuanza kazi ya
ujenzi wa soko hilo.
No comments:
Post a Comment