Mkuu wa wilaya ya Tanga Halima Dendego |
Na Rebeka Duwe.Tanga
MKUU wa shule ya MACECHU sekondari
iliyopo JijiniTanga,Melkisedeck Mzee ameuomba uongozi wa halmashauri ya Jiji
hilo kuipatia shule hiyo kuwapatia Daktari hali ambayo itasaidia kuwepo uhakika
wa tiba kwa wanafunzi 1040 ambao wamekuwa wakihudhuria masomo kwenye shule hiyo
yenye wanafunzi wa kutwa na bweni.
Ombi hilo limetolewa juzi wakati wa
hafla fupi ya makabidhiano ya msaada wa kompyuta ambao umetolewa na shirika la
KOICA msaada ambao umegharimu kiasi cha Tsh 22 milioni ambapo sasa wanafunzi wa
MACECHU sekondari wataweza kujifunza kisasa na katika ubora unaohitajika.
Kwa mujibu wa mkuu huyo wa shule ya
MACECHU,Mzee alisema kwamba wamepokea kompyuta mpya 20,ups 13,music system na
microphone ambapo hapo mwezi mei mwaka 2011walipokea kompyuta 20,ups
12,projector 1,air conditional na internet huku sehemu kubwa vikitumika kwa
wanafunzi.
Mkuu huyo wa sekondari ya MACECHU
aliendelea kusema kwamba mtaala huo wa KOICA umezingatia mahitaji ya shule hiyo
ambayo sasa inatimiza miaka kumi tangu kuanzishwa kwake huku ikifanikiwa
kufanya vizuri kitaaluma kwa mwaka 2013 kufaulisha wanafunzi 18 ambao
walikwenda kidato cha tano.
Alisema jitihada zao za kukuza
kiwango cha taaluma ndiyo siri pekee iliyowawezesha kuruhusiwa kupaqta hadhi ya
kuwa na kidato cha tano ambapo kwa mwaka huu mwezi jula waliweza kupokea
wanafunzi 65 wa mikondo ya CBG na PCB masomo ambayo yatasaidia kuzalisha
wataalam wa sayansi.
“Tumeamua kuchukua mchepuo wa
sayansi ili na sisi tuweze kutoa mchango wetu katika nchi kwa kupunguza tatizo la
wataalam wa sayansi kwenye Taifa,tunaishukuru serikali yetu na wadau mbalimbali
wanaotuunga mkono hadi kufanikiwa kufikia katika hatua hii”alisema mwalimu mkuu
wa MACECHU.
Pia mkuu huyo wa sekondari ya
MACECHU alibainisha kuwa mbali na KOICA kuwapatia vifaa hivyo ambavyo vitatoa
mchango mkubwa katika ufundishaji wa masomo ya sayansi lakini pia shirika hilo
la KOREA limeweza kuisaidia shule hiyo kwa kuwapatia walimu watatu
wanaofundisha kompyuta.
Aidha Mzee alisema kwamba shule hiyo
bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo tatizo la upungufu wa
madawati na viti madarasani,meza za chakula,meza za kusomea,vitabu vya kiada na
ziada huku pia kukiwepo na hitaji la maabara yenye kutosheleza idadi ya
wanafunzi waliopo hivi sasa.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya
Tanga Halima Dendego aliyekuwa mgeni rasmi kwenye shughuli hiyo ya upokeaji wa
msaada huo,alisema kwamba ipo haja kwa wanafunzi kujikita katika elimu ambapo
amewataka kuongeza jitihada za kusoma kwa bidii na maarifa njia itawasaidia
kutimiza ndoto zao.
Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba
katika kipindio hiki cha ushindani wa soko la ajira vijana wanahitajika kuwa
wasomi ambao wamebobea kwenye taaluma mbalimbali utaratibu ambao utawawezesha
kupambana vyema katika ushindani wa soko la ajira na mataifa mengine duniani.
No comments:
Post a Comment