HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Friday, 22 August 2014

HABARI ZA MATUKIO KUTOKA MWANZA NA LODRICK NGOWI



WAZAZI WATAKIWA KUWAPELEKA WATOTO KUPATA CHANJO YA SURUA

WAZAZI wametakiwa kushiriki kikamilifu kwa kuwapeleka watoto wao
kwenye vituo vya afya kwaajili ya kupata chanjo ili kuzuia magonjwa ya
surua paamoja na lubela.

Wito huo umetolewa na kaimu Afisa mtendaji wa kata ya Nyamagana Magret
Mtelele wakati akifanya mahojiano na wanahabari jana,na kuongeza
chanjo hiyo ni kwa watoto kuanzia miezi sita mpaka miaka kumi na nne.

“Kampeni hii itaanza mnamo tarehe 24 hadi 30 mwezi wa tisa,hivyo
nawaomba wazazi wajitokeze kwa wingi kuwaleta watoto wao ili waweze
kupata chanjo”alisema Mtelele.

Aidha alieleza kuwa kampeni hiyo inadhaminiwa na Halimashauri ya Jiji
la Mwanza  kwa kushirikiana na UNICEF na kuwa hawahitaji kadi za
kliniki za watoto hao bali wananchi wanapaswa kufika  kwenye vituo
hivyo vya afya kwa wakati wakiwa na watoto wao.

“Hatutahitaji kadi za kliniki,kwasababu wanaweza wakashindwa kuja kwa
kisingizio hicho,chamsingi wajitokeze kwa wingi ili watoto wao wapate
kinga dhidi ya magonjwa hayo”alieleza

Hata hivyo amewataka kina baba pia wanapaswa kushirikiana na wake zoa
kupeleka watoto wao katika vituo vya afya ili kuzuia magonjwa hayo
hatari kwa watoto.

JAMII ,SERIKALI VYOMBO VYA HABARI VYATAKIWA KUZUIA MMOMONYOKO WA MADILI

Naibu waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo
Mh.JUMA NKAMIA


SERIKALI kwa kushirikiana na vyombo vya habari,madhehebu ya dini
pamoja na jamii kwa ujumla zimeombwa kutunga sera itakayoisaidia jamii
kuhusiana na mavazi kwa lengo la kuiweka nchi katika maadili ya
kitanzania kwa kutoa muongozo kwa kizazi cha sasa.

Hayo yalisemwa na Ofisa utamaduni na michezo wa halmashauri ya jiji la
Mwanza juzi,Aika Lauwo huku akiitaka jamii kudumisha mila,desturi na
utamaduni wa mtanzania.

“naiomba serikali kushirikiana na vyombo vya habari,madhehebu ya dini
na jamii kwa ujumla kutunga sera ambazo zitasaidia jamii kuhusiana na
mavazi kwa lengo kuiweka nchi katika maadili mema ya
kitanzania”.alisema Lauwo.

Lauwo alisema kuwa mitandao ya kijamii ni chanzo cha mmomonyoko wa
maadili kutokana na vitu vinavyowekwa katika mitandao hiyo hatua
inayopelekea vijana kujiingiza zaidi katika ulevi,mapenzi na hivyo
kuchangia mmomonyoko wa maadili kwa kasi.

Aidha alieleza kuwa mmomonyoko wa maadili umekuwa ni tatizo kutokana
na wazazi na jamii kuacha maadili ya kitanzania na kujikita katika
usasa ambapo baadhi ya vijana huiga matendo na tabia za nje ya nchi
kupitia mitandao ya kijamii.

Hata hivyo aliwataka vijana wanaoingia katika mitandao ya kijamii
kufanya vitu vya maana badala ya kuangalia mambo ambayo hayawahusu na
pia waepuke matumizi ya vitu vinavyoharibu uasili wa maumbile yao.

No comments:

Post a Comment