Na Mwadishi Wetu(Handeni)
Watu 3 wa Familia Moja wamefariki Dunia baada ya kula
futari inayosadikika kuwa na sumu katika kijiji cha Kwasunga Wilayani Handeni
Mkoani Tanga.Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Tanga Costantine Masawe amewataja waliofariki kuwa ni Mwajuma Jumbe (3) Ramadhani Jumbe (5) na Abdi jumbe (7) .
Familia yenye Watu sita akiwemo Mzee Jumbe Mwenye umri wa miaka 40 na wake zake wawili waliweza kuwahishwa Hospitali ya Mkata kwa ajili ya kupatiwa matibabu na hatimaye kuruhusiwa kurudi nyumbani baada ya hali zao kuonekana kutengamaa.
Sambamba na hilo lakini pia katika kijiji cha Mwagodi Wilayani Mkinga Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Sambai Sangaire (37) ameuawa kwa kupigwa risasi na Majambazi akiwa Dukani kwake july 19 saa tatu usiku
No comments:
Post a Comment