HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Tuesday, 22 July 2014

KAMISHNA WA POLISI NA MKURUGENZI WA MAKOSA YA JINAI ZANZIBAR WAFUNGULIWA KESI MAHAKAMANI BAADA YA KUWAKAMATA WATU 8 NA KUWAHUSISHA NA MAKOSA YA MILIPUKO YA MABOMU





Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, Salum Msangi wamefunguliwa kesi mahakamani baada ya kuwakamata watu wanane na kuwahusisha na makosa ya milipuko ya mabomu ikiwamo kuwaweka kizuizini muda mrefu bila ya kuwafikisha mahakamani.

Katika kesi hiyo ya maombi Namba 7 ya mwaka 2014 imefunguliwa katika Mahakama Kuu ya Zanzibar iliyopo Vuga na imepangwa kuanza kusikilizwa Julai 21 mbele ya Jaji Mkusa Issack Sepetu na viongozi hao wametakiwa kujibu hati za kiapo kabla ya kesi hiyo kuanza kusikilizwa Jumatatu.

Kesi hiyo imefunguliwa na Wakili Abdallah Juma Mohamed akishirikiana na Rajab Abdallah Rajab kutoka Kampuni ya Mawakili ya AJM Solicitor ambao wanataka mahakama kuwaita viongozi hao ili waeleze mahali walipo wateja wanane wanaowatetea tangu walipokamatwa katika maeneo na nyakati tofauti visiwani Zanzibar.

Kwa mujibu wa hati hiyo ya kiapo watu hao ambao wanadaiwa kukamatwa na kuwekwa kizuizini ni Nassor Ahamad Abdallah, Mohamed Ishaq Yussuf, Said Kassim Ali, Hassan Bakari Suleiman, Rashid Ali Nyange Antar Homuod, Khamis Salum Amour na Salum Ali Salum.
Kesi hiyo ya maombi ilianza kutajwa jana na Wakili Abdallah Juma Mohamed alisema wamefungua kesi hiyo kwa kuzingatia Katiba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba ya Zanzibar ambavyo vinaelezea haki ya washtakiwa.
Mkuu wa Utawala wa Jeshi hilo Kamishna Msaidizi Mwandamizi Aziz Juma Mohamed ambaye alifika mahakamni kwa niaba ya Kamishna wa Polisi akiwa ameandamana na Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Salum Msangi alisema wako tayari kusikilizwa kwa ombi hilo.
Jaji Mkusa alisema kesi hiyo itasikilizwa Julai 21.


No comments:

Post a Comment