matumaini ya
Arsenal na Chelsea ya kumsajili Sami Khedira huenda yakawa yamepata pigo baada
ya Real Madrid kuwapa Monaco mchezaji huyo atakayenunuliwa kwa takriban pauni
milioni 20
Paris St-Germain
huenda wakashindwa kumsajili Paul Pogba, 21, kutokana na sheria za matumizi ya
fedha. Hali hiyo inatoa mwanya kwa Real Madrid na Manchester United zinazotaka
kumsajili
hatma ya Xherdan
Shaqiri haifahamiki baada ya mazungumzo ya kuhamia Liverpool kukwama. Kiungo
huyo wa Bayern Munich pia anasakwa na AS Roma na Juventus
Arsenal watatakiwa kutoa pauni milioni 24
kumsajili kiungo wa Sporting Lisbon William Carvalho, 22
Bayern Munich wapo tayari kutoa pauni milioni 33
kuwazidi kete Barcelona kumsajili Juan Cuadrado, 26, kutoka Fiorentina
beki wa Southampton Dejan Lovren, 25, anakaribia kukamilisha uhamisho wa pauni milioni 20 kwenda Liverpool wiki hii.
TETESI NYINGINEZO
Liverpool
wamemuulizia kiungo wa Real Madrid, Isco, 22, baada ya mabingwa hao wa Ulaya
kumsajili Toni Kroos na James Rodriguez kutoka Colombia (Daily Star),
Leicester
wanamfuatilia mshambuliaji kutoka Algeria Islam Slimani, 26, anayechezea Sporting
Lisbon (Daily Mail),
beki wa Manchester
City Micah Richards, 26, anataka kwenda kucheza kwa mkopo baada ya Tottenham,
Newcastle na Liverpool kukataa kutoa pauni milioni 7 (Daily Express),
mshambuliaji Didier
Drogba, 36, anakaribia kurejea Chelsea wakati mazungumzo kuhusu mkataba wa
mwaka mmoja yakiendelea (Daily Mail),
Tottenham
watamfuatilia kiungo Morgan Schneiderlin, 24, mara baada ya kukamilisha usajili
wa beki wa kushoto wa Swansea Ben Davies, 21 (Daily Mirror),
kuwasili kwa Davies
Tottenham kutafungua njia kwa Danny Rose kuhamia Hull City kwa pauni milioni 6
(Sun),
mkurugenzi mkuu wa
AC Milan Adriano Galliani amekanusha kupokea dau lolote kutoka Arsenal
kuhusiana na Mario Balotelli (Sky Sports),
Arsenal wamefikia
makubaliano ya pauni milioni 3.2 ya kumsajili kipa David Ospina , 25, kutoka
Nice (Le Figaro),
Real Madrid
wanataka kumsajili mshambuliaji wa Manchester City Alvaro Negredo, 28, kuziba
nafasi ya Alvaro Morata anayekwenda Juventus (Marca),
Chelsea wametoa
pauni milioni 20 kutaka kumsajili beki Miranda , 29, kutoka Atlètico Madrid
(AS.com),
meneja wa Napoli
Rafael Benitez anataka kumsajili Christoph Kramer, 23, kutoka Borussia
Moenchengladbach (L'Equipe),
Atlètico Madrid
wako makini kumsajili tena Fernando Torres na wameanza mazungumzo ya kutaka
kutoa pauni milioni 12.6 (Eurosport),
No comments:
Post a Comment