HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Thursday, 3 April 2014

RAIS JAKAYA KIKWETE AMTEUA PROFESA MARK MWANDOSYA KUWA MKUU WA CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA (MUST)


Rais Jakaya Kikwete (kulia)akiwa na
Profesa Mark Mwandosya

Rais Jakaya Kikwete amemteua Profesa Mark Mwandosya kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (Must) wakati Profesa Joseph Msambichaka akiteuliwa Makamu Mkuu wa chuo hicho.

Katika uteuzi huo uliofanyika mwishoni mwa Machi mwaka huu, Rais pia amemteua Profesa Osmund Kaunde kuwa Naibu mkuu wa chuo upande wa taaluma, utafiti na ushauri, wakati Profesa Emmanuel Luoga ameteuliwa kuwa Naibu Mkuu wa chuo atakayeshughulikia utawala, fedha na mipango.

Taarifa iliyotolewa jana na chuo hicho ilisema kuteuliwa kwa viongozi hao kunalenga kukiimarisha zaidi chuo ambacho kilipanda hadhi ya kuwa chuo kikuu tangu mwaka 2012.

Wakati huo huo, Uingereza inajivunia kuwa nchi inayoongoza katika uwekezaji nchini Tanzania na itaendelea kuisaidia Tanzania katika jitihada zake za kiuchumi na kuleta maendeleo.

No comments:

Post a Comment