![]() |
| Cristiano Ronaldo |
>>RONALDO
AIFIKIA REKODI YA MESSI BAO 14 MSIMU MMOJA UEFA CHAMPIONZ LIGI!
Real Madrid,
wakicheza Uwanjan kwao Santiago Bernabeu Jijini Madrid Nchini Spain, Usiku huu
wameichapa Borussia Dortmund Bao 3-0 katika Mechi ya Kwanza ya Robo Fainali ya
UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Gareth Bale ndie
aliefunga Bao la Kwanza katika Dakika ya 3 tu baada kuunganisha pasi safi ya
Daniel Carvajal na kumzidi akili Kipa Roman Weidenfeller
Bao la Pili la Real
lilifungwa katika Dakika ya 27 kupitia Isco kwa Shuti la chini toka Mita 20.
Hadi Mapumziko Bao
zilikuwa Real 2 Dortmund 0.
Katika Dakika ya 57,
Mchezaji Bora Duniani, Cristiano Ronaldo, alipiga Bao la 3 baada kumtoka Kipa
Roman Weidenfeller kufuatia kupokea pasi safi ya Luka Modric.
Hilo ni Bao la 14 kwa
Ronaldo kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu huu na ameifikia Rekodi ya Ronaldo ya
Lionel Messi aliefunga Bao 14 katika Mechi 11 za UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu wa
2011/12 wakati Ronaldo amechukua Mechi 8 tu.
Ronaldo hakumaliza
Mechi hii baada ya kuumia na kutolewa nje katika Dakika ya 80.
Timu hizi zitarudiana
huko Signal Iduna Park, Jijini Dortmund, Germany Jumanne Aprili 8.
CHELSEA YAPIGWA 3-1 NA PSG!
![]() |
| Javier Pastore |
Paris
Saint-Germain, wakicheza Uwanja wa kwao Parc des Princes huko Paris, France,
Usiku wa jana waliishinda Chelsea Bao 3-1 katika Mechi ya Kwanza ya Robo
Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Ezequiel
Lavezzi alitangulia kuwapa PSG Bao la kuongoza katika Dakika ya 4 baada kuweka
gambani Mpira uliookolewa kwa Kichwa na John Terry na kufumua Shuti moja kwa
moja na kumpita Kipa Petr Cech.
Chelsea
walisawazisha kwa Penati ya Dakika ya 27 iliyopigwa na Eden Hazard na ilitolewa
na Refa Milorad Mazic kutoka Serbia alipoamua Sentahafu wa PSG Thiago Silva
‘kamwangusha’ Oscar.
Hadi
Mapumziko Bao zilikuwa 1-1.
PSG
walifunga Bao lao la 2 baada ya Ezequiel Lavezzi kupiga Frikiki safi ambayo
Kipa Petr Cech alishindwa kuzuia na kumparaza Zlatan Ibrahimovic kisha Mchezaji
wa Chelsea David Luiz kuusindikiza wavuni.
Nchezaji
alietoka Benchi, Javier Pastore, aliipa PSG Bao la 3 katika Dakika ya 90 baada
ya kupokea Mpira wa kurushwa na kuwatoka Cesar Azpilicueta, Frank Lampard na
John Terry kisha kupiga Shuti la chini chini na kumshinda Kipa Petr Cech.
Timu
hizi zitarudiana huko Stamford Bridge Jumanne Aprili 8.


No comments:
Post a Comment