| Mtuhumiwa akijisalimisha kwa Polisi |
| Mkuu wa wilaya ya Chunya Deotatus Kinawiro Akizungumza na Wananchi wa Eneo hilo |
| ASKARI WA KIKOSI CHA KUTULIZA GHASIA WAKIWA ENEO LA TUKIO |
| WANANCHI WAKIMSIKILIZA MKUU WA WILAYA |
Wananchi
wa kijiji cha Chalangwa Kata ya Chalangwa alfajiri majira ya saa kumi wamefunga
barabara ya Mbeya kwenda Chunya baada ya Jeshi la Polisi kumkamata Mohammed
Katembo kwa kosa la kutishia kuua.
Baada
ya kukamatwa Katembo nyumbani kwake baada ya kufungwa pingu akiwa chini ya ulinzi
akidai sababu za kukamatwa kwake ilipigwa mbiu kijijini hali iliyopelekea
wananchi kujitokeza kwa wingi na kuamua kuifunga barabara hiyo huku mtuhumiwa
akitoroka akiwa na pingu mkononi.
Hali
hiyo ilisababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo wakiwemo
abiria waliokuwa wanakwenda na kutoka mikoa ya kaskazini,huku wananchi
wakimtaka Mkuu wa wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro aje kutatua mgogoro huo.
Mwenyekiti
wa kijiji Oscar Mwamwendesya amesema unatokana na mtu mmoja aliyefahamika kwa
jina la Joseph Mwazyele kupora eneo la mlima katika kijiji hicho bila taarifa
ya uongozi wa kijiji kupitia mkutano mkuu wa kijiji ambao ndio wenye dhamana ya
kutunza raslimali za kijiji.
Mkuu
wa wilaya ya Chunya Deotatus Kinawiro alilazimika kuingilia kati na kuifungua
barabara hiyo majira ya saa nne na nusu asubuhi kisha kukutana na wananchi wa
Chalangwa ambapo aliwataka kutoa kero zao ili kuupatia ufumbuzi mgogoro huo.
Wananchi
walidai kuwa Mwazyele amekuwa akitumia Polisi kwa kuwakamata wananchi wanaohoji
juu ya umiliki wa machimbo katika mlima kijijini hapo hivyo wamekuwa wakiishi
kwa hofu lakini pia hawjui uhalali wa umiliki wake kwa kuwa kijiji hakina
nyaraka zozote.
Katika
mkutano huo Mkuu wa Wilaya alipiga marufuku tabia za kujichukulia sheria
mkononi ikiwa ni pamoja na kufunga barabara na mauaji yaliyokithiri kijijini
hapo na wilaya ya Chunya kwa ujumla na Jeshi la Polisi limekuwa likifanya kazi
kubwa kudhibiti hali hiyo.
Aidha
amepiga marufuku shughuli zote za machimbo kijijini hapo na Mohammed Katembo
ajisalimishe na pingu za Polisi lakini wananchi walikataa wakidai afunguliwe
papo hapo ambapo Mtuhumiwa alijitokeza na kufunguliwa pingu mbele ya Mkuu wa
wilaya.
Mkuu
wa wilaya alimaliza kwa kuwataka wananchi kuchangia shilingi elfu mbili kwa
ajili ya uwanja wa kisasa wa michezo hali ambayo wananchi waliafiki na kukubali
kuchangia.
No comments:
Post a Comment