|
MWANAMKE
Mwanahawa Nassoro(32) Mkazi wa Mtaa wa Airport jijini Mbeya amehukumiwa
kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kupatikana na hatia ya
kunyanyasa na kumtesa mtoto.
|
Baba mzazi wa mtoto John akiwa amekaa na mwanae mara
tu baada ya hukumu kutolewa
|
MWANAMKE
Mwanahawa Nassoro(32) Mkazi wa Mtaa wa Airport jijini Mbeya amehukumiwa
kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kupatikana na hatia ya
kunyanyasa na kumtesa mtoto.
Mwanamke
huyo alipandishwa katika Mahakama ya Mwanzo ya Mbeya mjini juzi kutokana na
kosa lililokuwa likimkabili la kumtesa mtoto John Paul(03) ambaye ni
mtoto wa kaka yake.
Akisoma
mashitaka mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Mbeya mjini, Salome Mwakyosi,
mwendesha mashitaka wa Polisi Kopro Anthon alisema mtuhumiwa alitenda
kosa hilo Machi 12, Mwaka huu kwa nyakati tofauti kwa kumfungia ndani na
kumnyima chakula kinyume cha sheria namba 241 ya makosa ya jinai sura ya 16 ya
kanuni ya adhabu iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Alisema
Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Airport, Rehema Mohammed ndiye aliyebaini na
kutoa taarifa kwenye uongozi wa Mtaa ambapo mtuhumiwa alikamatwa na hatimaye
kufikishwa katika kituo cha Polisi kwa ajili ya hutua za kisheria.
Upande
wa Mashitaka ulikuwa na mashahidi wane, ambapo wawili kati yao ndiyo
waliotoa ushahidi ambao ni pamoja na Mjumbe wa Serikali ya Mtaa na Mtoto
aliyefanyiwa ukatili huo ambaye alimtambua mahakamani Shangazi yake Mwanahawa
licha ya kuwepo watu wengi.
Mtoto
huyo alifika mahakamani kutoa ushahidi baada ya afya yake kuimarika kutokana na
kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya.
Hakimu
alipomuuliza mtoto kuhusu mtu aliyekuwa akimpiga alimuonesha Mwanahawa mara
tatu ambapo alizidi kumuonesha Shangaza yake huyo.
Kwa
upande wake mtuhumiwa wa kesi hiyo alipoulizwa kuhusiana na kosa hilo alikiri
ambapo Hakimu aliridhika na ushahidi uliotolewa na pande zote mbili ikiwa ni
pamoja na kukiri kwa mtuhumiwa.
Kutokana
na ushahidi huo Mahakama hiyo na ilimtia hatiani mshitakiwa kwa kumuadhibu
kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela ili iwe fundisho kwa watu
wanaofanya vitendo vya kikatili dhidi ya watoto.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment