| MASHABIKI WA MBEYA CITY |
| DANNY LAYNGA WA COASTA AKIMILIKI MPIRA |
| WACHEZAJI WA COASTA UNION WAKIMPONGEZA MOHAMMED MIRAJI(10) KWA BAO SAFI |
| BOBAN AKIWA DIMBAN LEO |
| MASHABIKI WA COASTAL UNION |
Hatimaye
wabishi wa Mbeya City wamekubali kipigo cha pili katika Ligi Kuu Bara baada ya
kufungwa bao 2-0 na wenyeji Coastal Union. kwa Bao za Chipukizi Mohamed Miraji aliefunga
katika Dakika ya 80 na 92 na kuifanya Coastal kufikisha pointi 25 na kuikamata
Ruvu Shooting.
Mchezo huo ambao ulianza kwa kasi kwa timu zote
kushambuliana kwa zamu ambapo mpaka timu zote zinakwenda mnapumziko hakuna timu
iliyoweza kuona lango la mwenzie.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa timu zote
kuingia uwanjani hapo zikiwa zimefanya mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji wake
ambapo kwa upande wa Coastal Union waliwatoa Ally Iddy,Crispian Odulla na Ayoub
Yahaya ambao nafasi zao zilichukuliwa na Suleimani Selembe,Mohamed Mtindi,Yayo
Lutimba na Keneth Masumbuko.
Kwa upande wa Mbeya City waliwatoa Mwegane
Yeya,Jeremia John nafasi zao zilichukuliwa na Fransisi Casto na Richard Peter
ambao waliweza kucheza vema licha ya kushindwa kuibuka na ushindi kwenye mechi
hiyo.
Vikosi vilivyozeshwa leo kwa upande wa Coastal
Union iliwachezesha Shabani Kado,mbwana hamisi,abdi banda,juma nyoso,yusuph
chuma,jerry santo,Daniel lyanga,ally iddi,haruna moshi,crispian odulla na ayoub
yahya.
Kwa upande wa Mbeya City iliwachezesha Davidi
buruani,azizi sibo,hasan mwasapili,deogratis Julius,yusuph abdallah,Anthony
matogolo,mwagane yeya,steven mazand,paul nonga,jeremia john na peter mapunda.
No comments:
Post a Comment