>>>MNYAMA HOOI KWA MAAFANDE
VPL,
Ligi Kuu Vodacom, iliendelea Leo kwa Mechi mbili Jijini Dar es Salaam ambapo
Azam FC ilibanwa kwa Sare ya 2-2 walipocheza na Tanzania Prisons, Matokeo
ambayo yamewafanya Mabingwa Yanga waendelee kubaki kileleni, na Simba kukiona
cha mtema kuni walipochapwa Bao 3-2 na JKT Ruvu.
++++++++++++++++++++++++++
LIGI KUU
VODACOM
MATOKEO:
Jumapili
Februari 23
Simba
2 JKT Ruvu 3
Azam
FC 2 Tanzania Prisons 2
++++++++++++++++++++++++++
![]() |
| Kocha wa Simba Zdravko Logarusic |
SIMBA
2 JKT RUVU 3
Kwenye
Mechi iliyochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam JKT Ruvu Leo
iliwaendesha mchakamchaka Simba na kuwanyuka Bao 3-2.
Hadi
Mapumziko, JKT Ruvu walikuwa mbele kwa Bao 2-0 zilizofungwa na Hussein Bunu na
Penati ya Emmanuel Swita ambayo waliipata baada Henry Joseph kumchezea rafu
Amos Mgisa.
Katika
Dakika ya 53, Emmanuel Swita aliifungia JKT Ruvu Bao la 3 na kuwafanya waongoze
3-0 lakini Simba walicharuka na kupata Bao mbili zilizofungwa na Amisi Tambwe
Dakika ya 64 na 84, moja likiwa kwa Penati baada ya Bunu kumuangusha Amri
Kiemba.
JKT
Ruvu, licha ya kumaliza Mtu 10 baada ya Damas Makwaya kupewa Kadi Nyekundu
kwenye Dakika ya 72 baada Kadi za Njano mbili, walisema kidete na kulinda
ushindi wao.
| Logaruzic akiwa na Wachezaji Maozezini |
| Patashika kwenye lango la JKT Ruvu |
| Tambwe akimtoka Beki wa JKT Ruvu |
| Mashabiki wa Simba wakiwa hawaamini kinachotokea |
VIKOSI:
SIMBA: Yaw Berko, William
Lucian 'Gallas', Henry Joseph, Joseph Owino, Donald Mosoti, Jonas Mkude,
Awadh Juma, Said Ndemla, Amissi Tambwe, Amri Kiemba, Haruna Chanongo.
JKT
RUVU:
Shaaban Dihile, Damas Makwaya, Edward Charles, George Minja, Salum Mtaki,
Nashon Naftali, Amos Mgisa, Emmanuel Swita, Idd Mbaga, Hussein Bunu, Sosthenes
Manyasi
++++++++++++++++++++++++++

AZAM
FC 2 PRISONS 2
Huko
Azam Complex, Chamazi, kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam, Wenyeji Azam FC
waliikosa nafasi ya kutwaa uongozi wa Ligi toka kwa Yanga baada kutoka Sare ya
2-2 na Tanzania Prisons.
Hadi
Mapumziko Bao zilikuwa 0-0.
Prisons
ndio waliofunga Bao la Kwanza katika Dakika ya 47 kwa Frikiki ya Omega Seme na
Azam kusawazisha chapchap katika Dakika ya 49 kwa Bao la Aggrey Morris na
kupiga Bao la Pili Dakika moja baadae kwa Bao la Kipre Tcheche.
Haikuchukua
muda kwa Kipre Tcheche kupewa Kadi ya Njano ya Pili na hivyo kutolewa nje kwa
Kadi Nyekundu na hii iliwapa mwanya Prisons ambao hatimae kwenye Dakika ya 80
walisawazisha kwa Bao la Mpalile.
![]() |
| Benchi la Ufundi la Azam(Kalli Ongalla kushoto na Joseph Marius Omog) |
VIKOSI:
AZAM
FC:
Mwadini, David, Erasto, Moradi, Aggrey Morris, Bolou, Himidi, Abubakar Sure
Boy, John Bocco, Brian Omony, Kipre Tchetche
Akiba:
Aishi, Jabir, Mwaipopo, Mcha, Kone, Malika, Kelvin
TANZANIA
PRISONS:
Wilbeth Mweta, Salum Kimenya, Lauriun Mpalile, Nurdin Chona, Lugano Mwangama,
Jimmy Shoji, Godfrey Magetha, Omega Seme, Peter Michael, Frank Wiliam Muwi,
Fred Chudu .
Akiba:
Beno Kakolanya, Bryson Mponzi, Henry Mwalugala, Hamisi Maingo, Six Ally
Mwasekaga, Jumanne Elfadhili, Ibrahimu Isihaka.
RATIBA:
Jumatano
Februari 26
Azam
FC v Ashanti United
MSIMAMO:
NA
|
TIMU
|
P
|
W
|
D
|
L
|
GD
|
PTS
|
1
|
Yanga SC
|
17
|
11
|
5
|
1
|
29
|
38
|
2
|
Azam FC
|
17
|
10
|
7
|
0
|
19
|
37
|
3
|
Mbeya City
|
19
|
9
|
8
|
2
|
8
|
35
|
4
|
Simba SC
|
19
|
8
|
8
|
3
|
16
|
32
|
5
|
Kagera Sugar
|
19
|
6
|
8
|
5
|
1
|
26
|
6
|
Coastal Union
|
19
|
5
|
10
|
4
|
5
|
25
|
7
|
Mtibwa Sugar
|
19
|
6
|
7
|
6
|
0
|
25
|
8
|
Ruvu Shooting
|
18
|
6
|
7
|
5
|
-4
|
25
|
9
|
JKT Ruvu
|
19
|
7
|
1
|
11
|
-13
|
22
|
10
|
Prisons FC
|
17
|
3
|
8
|
6
|
-3
|
17
|
11
|
Mgambo JKT
|
19
|
4
|
5
|
10
|
-17
|
17
|
12
|
Ashanti United
|
18
|
3
|
5
|
10
|
-15
|
14
|
13
|
JKT Oljoro
|
19
|
2
|
8
|
9
|
-15
|
14
|
14
|
Rhino Rangers
|
19
|
2
|
7
|
10
|
-11
|
13
|


No comments:
Post a Comment