Thursday,
20 February 2014 00:48
>>MTINDO
MPYA ULAYA: TIMU ZA NYUMBANI HOI KWA SIKU YA PILI!
UEFA
CHAMPIONZ LIGI
MATOKEO:
Jumatano
Februari 19
AC
Milan 0 Atletico de Madrid 1
Arsenal
FC 0 Bayern Munich 2
++++++++++++++++++++++++++++++++++++

ARSENAL
0 BAYERN MUNICH 2
Kwenye
Mechi ambayo Kipindi cha Kwanza kilishuhudia Penati mbili kukoswa na Kadi
Nyekundu, Mabingwa Watetezi Bayern Munich wamefanikiwa kuichapa Arsenal
waliokuwa kwao Emirates Bao 2-0 katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya
Timu 16 ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Dakika
ya 8 Mesut Ozil aliangushwa na Boateng na Penati kutolewa lakini Penati hiyo
iliyopigwa hafifu na Ozil iliokolewa na Kipa Manuel Neuer ambae ni Rafiki wa
Ozil tangu utotoni.
Kwa
Ozil hiyo ni Penati yake ya Tatu mfululizo kukosa akichezea Klabu, nyingine
zikiwa Arsenal ilipocheza na Marseille kwenye Makundi ya UCL Msimu huu na kabla
wakati akiwa na Real Madrid.
Kwa
kawaida Wapiga Penati wa Arsenal ni Olivier Giroud na Mikel Arteta na wote
hawakuwamo kwenye Mechi hii.
Kwenye
Dakika ya 37 Toni Kroos alipenyeza pasi ya juu kwa Arjen Robben ambae
alichomoka na kuipita Difensi na kukontroli Mpira akimhadaa Kipa Wojciech
Szczesny ambae alimwangusha na Refa Nicola Rizzoli toka Italy kutoa Penati na
Kadi Nyekundu kwa Szczesny.
Lakini
David Alaba alikosa Penati hiyo iliyopiga Posti chini na kutoka huku Kipa wa
Akiba, Fabianski, alieingizwa baada kutolewa Santi Cazorla ili kukaa langoni
‘akienda mbovu’.
Katika
Dakika ya 54, baada kupokea pasi safi toka kwa Nahodha Philip Lahm, Toni Kroos
aliachia shuti toka Mita 20 ambalo lilipita juu kulia na kutinga wavuni na
kuwapa Byern Munich Bao safi.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++
TAKWIMU
MUHIMU-Toni Kroos v Jack Wilshere
-TONI
KROOS:
Pasi 152, 127 ndani ya Nusu
ya Uwanja upande wa Arsenal, ikiwa ni Asilimia 96.7% ya Pasi zilizokamilika
sahihi.
-JACK
WILSHERE: Pasi 33, Asilimia 66.7% sahihi.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Bayern
katika Dakika ya 88 baada ya pasi yake kuunganishwa kwa kichwa kilichodunda
chini cha Thomas Muller, alieingia Kipindi cha Pili, na kumhadaa Kipa
Fabianski.
Kwa
ushindi huu wa Bao 2-0, Mabingwa wa Ulaya Bayern Munich wamejiweka katika hali
njema kucheza Robo Fainali na Arsenal wanahitaji kushinda 3-0 huko Munich ili
wapindue kipigo.
Timu
hizi zitarudiana huko Allianz Arena Jijini Munich, Germany hapo Machi 11.
VIKOSI:
ARSENAL
(Mfumo 4-2-3-1): Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs;
Flamini, Wilshere; Ozil, Cazorla, Oxlade-Chamberlain; Sanogo.
Akiba:
Fabianski, Rosicky, Podolski, Giroud, Monreal, Jenkinson, Gnabry.
BAYERN
MUNICH (Mfumo: 4-1-2-3): Neuer; Boateng, Dante, Martinez, Alaba;
Lahm; Thiago, Kroos; Robben, Mandzukic, Gotze.
Akiba:
Starke, Van Buyten, Rafinha, Pizarro, Muller, Contento, Schweinsteiger.
Refa:
Nicola Rizzoli (Italy)
++++++++++++++++++++++++++++++++++++

AC MILAN
0 ATLETICO MADRID 1
Bao
la Dakika ya 82 kwa kichwa cha Straika hatari Diego Costa limewapa Atletico
Madrid ushindi wa Bao 1-0walipocheza Ugenini huko San Siro na AC Milan katika
Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Timu
hizi zitarudiana huko Estadio Vicente Calderon hapo Machi 11.
VIKOSI:
AC MILAN
(Mfumo 4-2-3-1): Abbiati, De Sciglio, Bonera, Rami, Bonera,
Emanuelson; Essien, De Jong; Poli, Kaká, Taarabt; Balotelli.
Akibas:
Amelia, Mexès, Abate, Constant, Zaccardo, Pazzini, Petagna.
ATLÉTICO
MADRID [Mfumo 4-4-2] : Courtois, Juanfran, Godín, Miranda,
Insua; Gabi, Mario Suárez; Koke, Raúl García, Arda Turan; Diego Costa.
Akiba:
Aranzubia, Alderweireld, Cristian Rodríguez, Sosa, Diego, Adrián López, Villa.
Refa:
Proença (Portugal)
UEFA
CHAMPIONZ LIG
Raundi
ya Mtoano ya Timu 16
MATOKEO:
Jumanne
Februari 18
Manchester
City 0 FC Barcelona 2
Bayer
04 Leverkusen 0 Paris Saint-Germain 4
RATIBA:
[Saa za
Bongo]
Jumanne
Februari 25
20:00
Zenit St. Petersburg v BV Borussia Dortmund
22:45
Olympiacos CFP v Manchester United
Jumatano
Februari 26
22:45
Schalke 04 v Real Madrid CF
22:45
Galatasaray Spor Kulübü v Chelsea FC
MARUDIANO
Jumanne
Machi 11
22:45
Bayern Munich v Arsenal FC
22:45
Atletico de Madrid v AC Milan
Jumatano
Machi 12
Jumatano
Machi 12
22:45
FC Barcelona v Manchester City
22:45
Paris Saint-Germain v Bayer 04 Leverkusen
Jumanne
Machi 18
22:45
Chelsea FC v Galatasaray Spor Kulübü
22:45
Real Madrid CF v Schalke 04
Jumatano
Machi 19
22:45
BV Borussia Dortmund v Zenit St. Petersburg
22:45
Manchester United v Olympiacos CFP
++++++++++++++++++++++++++++++++++
No comments:
Post a Comment