Hivi ndivyo ilivyokuwa ajali hiyo iliyohusisha Lori
na Coaster katika eneo la Mbalizi
|
Baadhi ya wananchi wakishuhudia ajali hiyo
iliyotokea majira ya saa 10:45 leo jioni katika eneo la Mlima Iwambi kuelekea
Mbalizi
|
Baadhi ya askari polisi wakilinda mali zilizokuwemo
katika Lori, hata hivyo askari hao walilazimika kurusha risasi hewani
kuwatawanya watu waliotaka kupora bidhaa hizo.
|
Mmoja wa majeruhi wa ajali akiwa katika hospitali
ya rufaa Mbeya akisubiri kupatiwa matibabu.
|
Wauguzi wa huduma ya haraka katika hospitali ya
Rufaa Mbeya wakimpatia huduma mmoja wa
majeruhi wa ajali hiyo |
WIMBI
la ajali katika miezi ya Disemba na Januari nchini limeendelea baada ya ajali
nyingine kutokea mkoani Mbeya leo jioni majira ya saa 10:45 katika mtelemko wa Mbalizi na kusababisha vifo vya
watu wawili na kujeruhi wengine 23.
Kwa
mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo ni kwamba magari mawili moja aina ya Coaster
na Lori la mizigo yalikuwa yakielekea njia ya Tunduma kutokea Jijini Mbeya
ambapo lori hilo linadaiwa kuharibika mfumo wa breki likiwa mtelemkoni.
Lori
hilo la mizigo aina ya SCANIA lenye namba za usajili T 101 CRL na trela lenye
namba za usajili T 859 BZW ambalo lilibeba bidhaa mbalimbali za madukani
liliigonga Coaster yenye namba za usajili T 910 BFB na kusababisha magari hayo
kupinduka.
Mashuhuda
hao walidai kuwa wakati Lori hilo likitelemka kwa kasi katika mlima huo mbele
yake kulikuwa na gari aina ya Toyota Hilux lenye namba za usajili T 370 AST
ambalo lilikuwa likipandisha mlima na hivyo kumchanganya dereva ambaye
alijikuta akiigonga Coaster kwa nyuma.
Mmoja
wa askari wa Usalama barabarani aliyekuwepo eneo la tukio alidai kuwa
wameshuhudia watu wawili waliokufa papo hapo na abiria wengine 23 wamekimbizwa
katika hospitali ya Rufaa Mbeya na Hospitali Teule ya Ifisi kwa ajili ya
matibabu.
Kwa
upande wake Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Barakael Masaki alithibitisha
kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa watu wawili ambao ni mwanamke na mwanaume
mmoja ambao majina yao hayajatambuliwa walifariki dunia katika ajali hiyo.
Aidha
katika hali isiyo kuwa ya kawaida askari wa kutuliza ghasi walilazimika
waliofika katika eneo la ajali walilazimika kufyatua risasi za moto hewani kwa
nia ya kuwatawanya watu waliofika katika eneo la ajali na kutaka kupora bidhaa
zilizokuwemo ndani ya lori.
No comments:
Post a Comment