HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Friday, 13 December 2013

SIMBA YASAJILI WAWILI " KIPA IVO MAPUNDA NA BEKI MKENYA DONALD MOSOTI OMWANWA




Na Godwin Lyakurwa
IVO ASAINI MIAKA MIWILI SIMBA SC
KIPA namba moja wa Tanzania, Ivo Philip Mapunda, usiku wa kuamkia leo amesaini Mkataba wa mwaka mmoja na nusu kujiunga na klabu ya Simba SC ya Dar es Salaam, akitokea Gor Mahia ya Kenya.
Ivo anasaini Simba SC, baada ya kung’ara akiwa na kikosi cha Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge mwaka huu.
Ivor Mapunda

Ivo aliiongoza Kilimanjaro Stars kufika Nusu Fainali ya Challenge baada ya kuwatoa waliokuwa mabingwa watetezi Uganda ‘The Cranes’ kwa penalti 3-2 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90, kipa huyo akicheza mikwaju miwili. 
Akizungumza baada ya kusaini Simba SC, Ivo alisema kwamba ameamua kusaini timu hiyo Mtaa wa Msimbazi baada ya kuridhishwa na maslahi aliyopewa.
Ivo Mapunda akisaini mbele ya Katibu wa Simba SC, Wakili Evodius Mtawala  
Ivo alisema kwamba Simba SC ni timu kubwa na anaamini atafanya vizuri.
“Sina wasiwasi, mimi ni kipa mzoefu na hata Watanzania wanajua uwezo wangu, baada ya kusaini, sasa ni kazi tu, kikubwa naomba ushirikiano na benchi la Ufundi, uongozi, wachezaji wenzangu na mashabiki na wadau kwa ujumla, ”alisema Ivo aliyewahi kudakia Yanga SC. 
Ivo Philip Mapunda alizaliwa Novemba 14, mwaka 1979 na kisoka aliibukia katika klabu ya Tukuyu Stars kabla ya kuhama Prisons zote za Mbeya, baadaye Moro United mwaka 2005 kabla ya kutua Yanga msimu uliofuata, 2006.
Aliidakia Yanga hadi 2009 akahamia St George ya Ethiopia alikopiga kazi msimu mmoja, akarejea nyumbani kuidakia African Lyon 2011 kabla ya 2012 kuhamia Bandari ya Mombasa, Kenya ambako alifanya kazi kwa miezi sita akasajiliwa na Gor Mahia.
Ivo anamaliza Mkataba wake Gor Mahia Desemba 16, mwaka huu na ataidakia kwa mara ya mwisho klabu hiyo katika mechi ya Kombe la DSTV Desemba 14 dhidi ya Tusker FC na baada ya hapo atapakia kila kilicho chake na kuja kuanza maisha mapya Msimbazi. 

Wakati huohuo SIMBA SC leo imefanikiwa kumsainisha Mkataba wa miaka miwili, beki wa kati wa klabu ya Gor Mahia ya Kenya, Donald Mosoti Omwanwa, ambaye ni pendekezo la kocha wa timu hiyo, Mcroatia, Zdravko Logarusic pamoja na kipa Ivo Mapunda.
Katibu wa Simba SC, Wakili Evodius Mtawala alitua jana usiku Nairobi na leo mchana akamsainisha Mkataba wa miaka miwili mchezaji huyo, mbele ya mchumba wake, Lilian Atieno.

Donald Mosoti Omwanwa akisaini mbele ya Katibu wa Simba Wakili Evodius Mtawala leo(picha na Bin Zubeiry blog)

Akizungumza baada ya kusaini Mkataba huo, beki huyo mrefu alisema kwamba anashukuru kujiunga na Simba SC, kwani ni klabu kubwa na ya kihistoria Afrika Mashariki.
“Nimefurahi kusaini Simba SC, hii ni klabu kubwa na ya kihistoria ukanda huu wa Afrika Mashariki, nataka kufuata nyayo za Wakenya wengine waliochezea klabu hii kwa mafanikio kama Mark Sirengo, Hillary Echesa na Mike Barasa,”alisema.
Mchezaji huyo anayetarajiwa kuondoka kesho kwenda Dar es Salaam kujiunga na wenzake, alisema kwamba amefurahi pia kwenda kufanya kazi tena chini ya kocha Logarusic, ambaye alikuwa mwalimu wake Gor Mahia.


“Mimi binafsi kama mchezaji ni faraja kwenda kufanya tena kazi na Loga, ni kocha mzuri na aliifanya Gor iwe na heshima hapa (Kenya) na hata Simba SC wajue wamepata kocha mzuri,”alisema.
Donald Mosoti Omanwa alizaliwa Julai 14, mwaka 1981 kijiji cha Kisii, Nyanza nchini na Kenya na alipata elimu yake ya Msingi na sekondari huko huko Kisii.
Kisoka, baada ya mpira wa shule, beki huyo alianzia klabu ya World Hope ya Nairobi mwaka 2005 kabla ya kuhamia Nairobi City Stars mwaka 2008 ambako alicheza hadi mwaka 2011 alipojiunga na Gor Mahia.
Omwanwa alisema Mkataba wake wa sasa na Gor Mahia unamalizika Februari 31, mwakani lakini ameruhusiwa kusaini Simba SC kwa kuwa Ligi ya Kenya inaanza Machi mwakani.
“Hakuna tatizo, Simba watapatiwa ITC (Hati ya Uhamisho wa Kimataifa) na nitacheza Tanzania,”alisema beki huyo aliyewahi kuichezea Kenya, Harambee Stars mechi moja tu dhidi ya Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’ ya kirafiki ya kimataifa iliyokuwa katika kalenda ya FIFA.       
Baada ya kumsaini beki huyo, Simba SC iko katika hatua za mwisho za kumalizana na Ivo Mapunda, aliyemaliza Mkataba wake Gor Mahia.


No comments:

Post a Comment