Na Godwin Lyakurwa Tanga
Taasisi za Serikali na zisizo za
Kiserikali Mkoani Tanga zimetakiwa kutoa ushirikiano wa kutosha katika Masuala
yanayohusu Utafiti,Ushauri na Elimu kwa Chuo Kikuu Huria Kituo cha Mkoa wa
Tanga ili kuweza kufanikisha shughuli za kimaendeleo kwa urahisi zaidi Mkoani
hapa.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa
Chuo Hicho Bi RAHMA MOHAMMED wakati akizungumza na Wanahabari Dec29 Chuoni hapo,
ambapo ameeleza kuwa Chuo hicho kimekuwa hakipewi hadhi na Ushirikiano wa
kutosha kutoka kwa wanajamii na Taasisi mbalimbali Mkoani hapa.
Akielezea Historia ya Chuo hicho Bi
Rahma amesema kuwa kilianzishwa kama moja kati ya zaidi ya vituo 30 vya Chuo
kikuu Huria cha Tanzania vilivyoko nchini , ambapo kilianzishwa Mwaka 2000
katika majengo Veta kikiwa na wanafunzi 53 hadi 1005 mwaka huu wa masomo
2013/2014 ambapo tangu mwaka 2018 mpaka sasa kinafanya shughuli zake katika
majengo ya TUKTA jijini Tanga.
Akielezea mafanikio ya Chuo hicho Bi
Rahma ameeleza kuwa Chuo kimefanikwa kudahili wanafunzi kutoka 53 mpaka 1001
kwa mwaka 2000/2013.Pia kimefanikiwa kuongeza wahitimu kutoka 53 kwa mwaka 2011
mpaka 101 kwa mwaka 2013.
Kwa upande wa Kafanikio amesema kuwa
Chuo kimefanikiwa kuanzisha Vituo katika Wilaya zote za Mkoa wa Tanga, Chumba
maalum cha Computer chenye Computer 10 zilizounganishwa kwenye Mtandao wa
Enternet ambapo wanafunzi huweza kujisomea na kupata taarifa kwa njia ya
mtandao bure,kuongeza miundombinu ya kutoa taaluma bora kupitia michango ya
wanafunzi kama Viti 40 na kujenga banda la kusomea wanafunzi.
Aidha Mkurugenzi huyo amebainisha
Changamoto mbalimbali zinazo kikabili chuo hicho kuwa ni pamoja na Ardhi kwa
Ajili ya kujenga Majengo maalum yatakayokuwa mali ya Chuo hicho.
“Tunachangamoto ya uhaba wa Ardhi kwa
ajili ya kujenga Majengo yetu Wenyewe ambapo tuliomba eneo na kupewa Eneo
Wilaya ya Muheza katika Eneo la Kilapura lakini lilivamiwa na Wanachi kabla
hatujamilikishwa hivyo Halmashauri ya Wilaya ya Muheza ikatukahamisha katika eneo jingine lililoko
Kibanda na tnasubiri Taratibu za kukabidhiwa”Alisema Bi Rahma.
Hata hivyo Mkurugenzi huyo ameeleza
kuwa bado si bora sana kupata eneo nje ya mji kwa sababu itakuwangumu kupata
mawasiliano kutoka Mkongo wa mawasiliano wa Taifa.
Akielezea Changamoto nyingine Bi Rahma
amesema kuwa uelewa finyu kwa Wananchi walioko mkoani Tanga hasa kwa kufikiri
kuwa Taaluma inayotolewa Chuoni hapo kuwa si nzuri kama ile inayotoka katika vyuo
vya bweni kitu ambacho si kweli, hali ambayo imesababisha Chuo hicho kushindwa
kufikia Malengo ya Udahili mwaka hadi mwaka.
Amesema pia uhaba wa kifedha kwa
ajili ya kufika katika maeneyo ya Vijijini kwa ajili ya kuwaelimisha na
kuwatangazia wanachi juu ya Ubora wa kutumia Chuo kikuu Huria kituo cha Mkoa wa
Tanga.
Bi Rahma amesema kuwa hali hiyo
imepelekea baadhi ya Kozi zinazotolewa Chuoni hapo kutotambulika na baadhi ya
Taasisi za Kiserikali Mkoani hapa akitolea Mfano Walimu zaidi ya 30 waliohitimu
Kozi ya Diploma Kituoni hapo na wanafanya kazi Wilayani Tanga mwajiri wao(TSD)
amekataa kuwapandisha madaraja na kuwataka warejeshe Barua walizochukua kwa
ajili ya kupandishwa Daraja kwa sababu ya kutoitambua kozi hiyo jambo ambalo
linashangaza na linarudisha nyuma maendeleo ya Chuo hicho kwa baadhi ya
wanafunzi wanaosoma kozi hizo kwa sasa kujitoa katika Kozi hiyo.
Nae Raisi wa Chuo hicho EUSTARD RWEGOSHORA
mesema kuwa wanashukuru Uongozi wa Chuo hicho kwa Ushirikiano mkubwa walionao
kwa wanafunzi wa Chuo hicho.Pia amesema kuwa wamejipanga vyema kuongeza
miundombinu ilikukidhi mahitaji ya
Wanafunzi wapya wanaoongezeka kila mwaka chuoni hapo hasa Viti na Vyumba
vya kusomea.
|
Rais wa Chuo hicho Ndg Eustard Rwegoshora(kushoto)Mkurugenzi
Msaidizi wa Chuo hicho Bi Rahma Mohammed(katikati) na Katibu wa Chuo Ndg Ahmed
Ngereza wakizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani)
|
|
Chumba Maalum cha Kompyuta
|
|
Maktaba ya Chuo hicho
|
No comments:
Post a Comment