>>NI MCHEZAJI WA PILI KUMSAINI DIRISHA DOGO LA
USAJILI!
MABINGWA wa Tanzania Bara, Yanga, wamethibitisha kumsaini
Kiungo kutoka Ruvu Shooting, Hassan Saleh Dilunga, kwa Mkataba wa Miaka
mitatu.
Dilunga ni Mchezaji wa pili kusainiwa na Yanga katika
Dirisha la Usajili lililofunguliwa rasmi leo Novemba 15 na litadumu hadi
Desemba 15 na Mchezaji mwingine ni Kipa Juma Kaseja ambae alikuwa Mchezaji huru
baada ya kumaliza Mkataba wake na Simba.
Akithibitisha Usajili huu wa Dilunga, Mwenyekiti wa Kamati
ya Usajili wa Yanga, Abdallah Bin Kleb, amesema usajili huu ni kutekeleza
maagizo ya Kocha Mkuu Ernie Brandts, ambae sasa yuko Likizo fupi huko kwao,
aliyoyaacha kabla kwenda Mapumziko.
Bin Kleb amesema: "Kocha aliacha mapendekezo ya usajili
tuyafanyie kazi la kwanza lilikuwa ni kuhakikisha tunampata Juma Kaseja kwa
ajili ya kuongeza nguvu katika nafasi ya Makipa ambalo tulilikamilisha mwishoni
mwa Wiki na sasa tumelimaliza la Kiungo Hassan Dilunga"
Hadi sasa Yanga ndio Vinara wa Ligi Kuu Vodacom baada ya
kukamilika Raundi ya Kwanza na Raundi ya Pili itaanza hapo Januari 25.
LIGI KUU VODACOM
MSIMAMO:
|
NO
|
TEAMS
|
P
|
W
|
D
|
L
|
GF
|
GA
|
GD
|
PTS
|
|
1
|
Young Africans
|
13
|
8
|
4
|
1
|
31
|
11
|
20
|
28
|
|
2
|
Azam FC
|
13
|
7
|
6
|
0
|
23
|
10
|
13
|
27
|
|
3
|
Mbeya City
|
13
|
7
|
6
|
0
|
20
|
11
|
9
|
27
|
|
4
|
Simba SC
|
13
|
6
|
6
|
1
|
26
|
13
|
13
|
24
|
|
5
|
Kagera Sugar
|
13
|
5
|
5
|
3
|
15
|
10
|
3
|
20
|
|
6
|
Mtibwa Sugar
|
13
|
5
|
5
|
3
|
19
|
17
|
2
|
20
|
|
7
|
Ruvu Shootings
|
13
|
4
|
5
|
4
|
15
|
15
|
0
|
17
|
|
8
|
Coastal Union
|
13
|
3
|
7
|
3
|
10
|
7
|
3
|
16
|
|
9
|
JKT Ruvu
|
13
|
5
|
0
|
8
|
10
|
16
|
-6
|
15
|
|
10
|
Rhino Rangers
|
12
|
2
|
4
|
6
|
9
|
16
|
-7
|
10
|
|
11
|
JKT Oljoro
|
13
|
2
|
4
|
7
|
9
|
19
|
-10
|
10
|
|
12
|
Ashanti United
|
13
|
2
|
4
|
7
|
12
|
24
|
-12
|
10
|
|
13
|
Tanzania Prisons
|
12
|
1
|
5
|
6
|
6
|
16
|
-10
|
8
|
|
14
|
Mgambo JKT
|
13
|
1
|
3
|
9
|
3
|
23
|
-20
|
6
|
RATIBA
RAUNDI YA PILI
25 Januari 2014
Ashanti United v Yanga
Azam FC v Mtibwa Sugar
Coastal Union v JKT Oljoro
Kagera Sugar v Mbeya City
Tanzania Prisons v Ruvu Shootings
JKT Ruvu v Mgambo JKT
Simba v Rhino Rangers


No comments:
Post a Comment