HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Monday, 25 November 2013

WATUMISHI MAFISADI MUHEZA KUKIONA CHA MOTO


Mkuu wa Wilaya ya Muheza Subira Mgallu

KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), imesema baadhi ya watumishi wa halmashauri wamekuwa wakijenga majumba na kutembelea magari ya kifahari kutokana na fedha zinazopaswa kupelekwa kwa wananchi kila mwaka kuzifisadi hatua ambayo sasa kamati hiyo imesema basi.
Sambamba na hilo, kamati hiyo imekataa hatua ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza kutumia fedha hizo zinazotokana na mapato ya ndani kupunguza makali ya kero ya maji, ikisema serikali imetoa mwongozo huo, ili wananchi waweze kupunguza umasikini.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Rajabu Mbarouk Mohamed, alisema kuanzia mwaka 2010 hadi 2013 sh milioni 229 hazikupelekwa kwa makundi ya wanawake na vijana kama ambavyo serikali ilielekeza.
“Hizi fedha zipo wapi ambazo katika mapato yenu ya ndani mnatakiwa kutoa asilimia tano ya kile mnachokikusanya kwenda kwa wanawake na vijana, lakini hamkufanya hivyo, mmekula fedha hizo,” alisema mwenyekiti huyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Ibrahim Matovu alipotakiwa kujibu fedha hizo zilipo, ingawa alijitahidi kuelezea namna walivyozitumia kutatua kero ya maji, lakini mwenyekiti alimkatisha akieleza kwamba madiwani wa CCM katika wilaya hiyo hawataki kushinda tena kwenye uchaguzi kutokana na kwamba waliowachagua ndio hao hawawatendei haki kwa kuwapelekea fedha zao.
Mwenyekiti huyo alimsimamisha ofisa maendeleo wa wilaya hiyo, Vije Mfaume ambaye ni katibu wa kamati inayopaswa kugawa fedha hizo kwa makundi hayo, lakini hata hivyo alijiumauma asijue atoe jibu gani, hadi mwenyekiti kumtoa nje ya kikao chake.
“Wewe ndio ofisa maendeleo ya jamii wa wilaya, umekaa hapa kwa miaka mingi lakini unashindwa kuwatendea haki watu hawa hata kama madiwani wa CCM hawaoni, lakini toka nje ya kikao changu, na kwanini kamati ya nidhamu isikujadili kwa kupata mshahara wa bure bila kuufanyia kazi,” alihoji mwenyekiti huyo na kuongeza.
“Madiwani wa CCM mnawasaliti wananchi wanawake ambao ndio wapiga kura muhimu sana hapa nchini, pia vijana ambao kundi hili lingepewa fedha hizo wangebuni wenyewe miradi ya kuwaingizia kipato, kama CCM ipo tayari kuona watu wake wanakikosesha kura 2015 kwa sababu ya kushindwa kupeleka fedha hizi kwa wapiga kura wake,” alisema.
Mjumbe wa kamati hiyo, Felister Bullah (Mbunge wa Viti Maalumu), alisema kuna vijana wengi wamefungwa jela kwa sababu ya kutuhumiwa kuiba kuku, kuiba nguo, lakini endapo fedha hizi zingepelekwa zingewasaidia kuepukana na hali hiyo.
Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugora, alisema fedha hizo mara nyingi wakurugenzi wamekuwa wakizifanyia miradi wakati serikali iliona umasikini unashika kasi kwa makundi mengi hapa nchini, na kuunda mifuko ya vijana na wanawake kupitia halmashauri zao, ili iweze kuwasaidia kupunguza umasikini.
“Fedha hizi wakurugenzi wanazifanya ni miradi yao, wanajenga maghorofa, wanatembelea magari ya kifahari, wanashika simu za bei mbaya, lakini sasa tunataka kamati hii ikomeshe hali hii,” alisema Lugora.
Baada ya maelezo hayo, mwenyekiti alimwagiza Mkuu wa Wilaya, Subira Mgalu kutumia sheria yake ya kuwaweka ndani saa 24 watu wanaokwenda kinyume, kwa kuwaweka ndani mkurugenzi, mweka hazina, Amina Kipindullah na ofisa maendeleo ya jamii kwa kupoteza fedha hizo za wananchi.
Hata hivyo, mkuu huyo wa wilaya aliikingia kifua halmashauri yake kwa kueleza kwamba kama ni kuwekwa ndani, basi itabidi ajiweke yeye mwenyewe kwa kuwa pia alishiriki kutumia fedha hizo kutatua kero ya maji katika mji wa Muheza ambao kuna kipindi Mkuu wa Majeshi, Aden Mwamunyange, aliwasaidia gari la jeshi kuleta maji kuwasaidia wananchi.
Credit:Tanzania Daima

No comments:

Post a Comment