HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Monday, 25 November 2013

TANGA YAZIZIMA KWA MAJONZI 'WATU 7 WAFA KATIKA AJALI YA BARABARANI"



Kamanda Massawe

Tanga.
Watu saba wamekufa papo hapo na wengine 21 kujeruhiwa vibaya katika eneo la Chang’ombe, Barabara ya Segera – Chalinze, wilayani Korogwe, Tanga baada ya mabasi mawili madogo ya abiria waliyokuwa wakisafiri kugongana uso kwa uso.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Constantine Massawe alisema jana kwamba ajali hiyo ilitokea juzi saa 10:20 jioni baada ya gari moja kukwepa mbuzi waliokuwa wameingia barabarani.

Alisema majeruhi wamelazwa katika Hospitali ya Magunga.
Alisema kati ya waliofariki, watatu walitambulika majina yao akiwemo dereva wa moja ya mabasi hayo aliyefahamika kwa jina moja la Kombo. 

Wengine ni mkazi wa Muheza, Martin Simon (35) na mkazi wa Korogwe, Juma Abdallah (37).
Aliwataja waliojeruhiwa kuwa ni Valerian Richard (27), Mohamed Juma (60), Halima Abbas (35), Ali Rashid (61),  Asha Bakari (39), Rehema Hassan (39), Ibrahim Ramadhan (26), Omari Issa (30), Issa Ibrahim (30) na Shaaban Hamza(35)

Wengine ni Ramadhan Mdangula (30), Mwanahawa Selemani (25), Mariam Ramadhan (24), Theresia Gabriel (35), George Ernest (25), Issa Mohamed (32), Fatma Hassan (48), Sharifa Bano (40), Shida Bano (27), Abel Elia (35), Fadhil Rajabu (28) na mwingine aliyefahamika kwa jina moja la Marijani.

No comments:

Post a Comment