WATU watano wamekufa papo hapo kwenye ajali mbaya
iliyotoka leo alfajiri katika kijiji cha Dakawa - Sokoine Wilaya ya Mvomero
mkoani Morogoro. Ajali hiyo iliyohusisha gari ya abiria aina ya Noah yenye
namba za usajili T 502 AUP iliyokuwa ikitoka Wilaya ya Gairo kuelekea Morogoro
mjini kugongana uso kwa uso na lori aina ya Scania lenye namba za usajili T129
AGB ambalo lilikuwa likitoka Dar es Salaam kuelekea Tabora.
Watu hao wamepoteza maisha katika ajali huyo akiwemo dereva wa Noah aliyejulikana kwa jina la Masoud Juma na wengine wanne hali zao ni mbaya.
"Chanzo cha ajali hii ni dereva wa Noah ambaye alikuwa akijaribu kulipita gari lililokuwa mbele yake na ghafla akakutana na lori uso kwa uso" alisema Bw. Sanjo Ole ambaye ni mfugaji jamii ya Kimasai.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile amedhibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

No comments:
Post a Comment