![]() |
| The TANZANITE |
KIKOSI cha timu ya soka ya taifa ya wanawake chini
ya miaka 20 (Tanzanite) kinaagwa kesho (Novemba 6 mwaka huu) saa chache kabla
ya kuanza safari ya kwenda Maputo, Msumbiji.
Hafla fupi ya kuikabidhi bendera Tanzanite itafanyika kesho saa 5 asubuhi kwenye ofisi za TFF wakati kikosi hicho kinatarajiwa kupaa saa 11 jioni kwa ndege ya LAM na kuwasili Maputo saa 3.45 usiku.
Msafara wa Tanzanite ambayo ilishinda mechi ya kwanza mabao 10-0 karibu wiki mbili zilizopita jijini Dar es Salaam utaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Kidao Wilfred.
Mechi hiyo ya marudiano itachezwa Novemba 9 mwaka
huu Uwanja wa Taifa wa Zimpeto, na timu itarejea nyumbani Novemba 10 mwaka huu
saa 8.30 mchana kwa ndege ya LAM.
Wakati huohuo
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetuma
waraka kwa vyama vya mpira wa miguu vya wilaya, mikoa na vyama shiriki kuvitaka
kuwasilisha orodha ya wote waliofaidika na msamaha wa Oktoba 28 mwaka
huu.
Oktoba 28 mwaka huu wakati akizungumza katika Mkutano
Mkuu baada ya uchaguzi, Rais mpya wa TFF, Jamal Malinzi alitoa msamaha kwa wote
waliofungiwa kwa sababu mbalimbali.
Hata hivyo, msamaha huo hauwahusu waliofungiwa kutokana
na makosa ya rushwa au kupanga matokeo. Vilevile haugusi adhabu zilizotolewa
ndani ya klabu.
Vyama vya mikoa vinatakiwa kuhakikisha waraka huo
unafika kwa wanachama wao (vyama vya mpira wa miguu vya wilaya). TFF inataka
orodha ya wote waliofaidika na msamaha huo kwa ajili ya kumbukumbu zake
(records).


No comments:
Post a Comment