ASHANTI
UTD, SIMBA UWANJANI VPL
Mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zinaanza kesho (Novemba 6 mwaka huu) ambapo Ashanti United itakuwa mwenyeji wa Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
| Simba Sport Club |
| Ashanti United |
Viingilio
katika mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 10 kamili chini ya mwamuzi Andrew
Shamba kutoka Pwani ni sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Waamuzi
wasaidizi ni Abdallah Mkomwa na Rashid Abdallah wote kutoka Pwani wakati mezani
atakuwa Hamisi Chang’walu.
Mechi
nyingine za kesho ni JKT Ruvu Stars na Coastal Union (Uwanja wa Chamazi),
Kagera Sugar na Mgambo Shooting (Uwanja wa Kaitaba, Bukoba) na Ruvu Shooting na
Mtibwa Sugar (Uwanja wa Manungu, Morogoro).
| Coastal Union "Wagosi wa Kaya" |
Keshokutwa
(Novemba 7 mwaka huu) raundi ya 13 kumaliza mzunguko wa kwanza itakamilika kwa
mechi kati ya Yanga na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa kwa viingilio vya sh.
5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
![]() |
| Azam Fc |
![]() |
| Mbeya City "Wazee wa amsha Popo" |
Azam itakuwa mwenyeji wa Mbeya
City kwenye Uwanja wa Chamazi wakati Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora
utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Rhino Rangers na Tanzania Prisons kutoka
Mbeya.
![]() |
| Kikosi ya Yanga |
Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Rhino itakuwa mwenyeji wa Tanzania
Prisons.




No comments:
Post a Comment