Kutoka Visiwani
Mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Chanel Ten anayefanyia
kazi hapa Zanzibar Munir Zakaria, ametishia kumpandisha mahakamani kocha mkuu
wa Zanzibar Heroes Salum Bausi iwapo hatamuomba radhi kwa madai kuwa kocha huyo
amemdhalilisha kwa kummwagia matusi ya nguoni hadharani.
Zakaria
alikumbwa na kadhia hiyo jana asubuhi, wakati alipokwenda uwanja wa Mao Tse
Tung kufuatia mazoezi ya Zanzibar Heroes kwa ajili ya kuripoti kwenye kituo
chake anachofanyia kazi, ambapo kocha Bausi aliamua kumshambulia kwa maneno,
akionesha kukerwa na suala la mwandishi huo alilomuuliza Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein Ikulu Jumanne
iliyopita.
Katika
mkutano wa Mheshimiwa Rais na waandishi wa habari, Zakaria alidai kuwa, Rais
ndiye aliyeiambia ZFA imrejeshe Bausi kuifundisha timu hiyo, wakati wananchi na
baadhi ya wachezaji hawamtaki, jambo ambalo Rais alikanusha na kutoa ufafanuzi
juu ya alichosema siku alipotembelewa na ujumbe wa Wazee SC akiwemo Rais wa ZFA
Ravia Idarous.
Kufuatia mashambulizi hayo ya maneno na kutimuliwa uwanjani hapo, Zakaria amemwambia mwandishi wa habari hizi aliyeshuhudia kadhia hiyo, kuwa anampa Bausi siku saba kuomba radhi, vyenginevyo atampandisha kizimbani kudai fidia ya kuvunjiwa heshima kadamnasi, na kwamba anaendelea kujadiliana na mwanasheria wake.
![]() |
| Humud |
Wakati
huohuo,Kiungo wa timu ya Taifa ya Zanzibar ‘The Zanzibar
Heroes’ Abdulhalim Humoud, ametimuliwa katika kikosi hicho baada ya kushindwa
kuripoti kambini na wenzake.
Taarifa
zilizopatikana na mwandishi wa habari hizi jana, zimefahamisha kuwa, mchezaji
huyo aliyesajiliwa na Simba SC ya Dar es Salaam, ambaye alikuwa Zanzibar
akifanya mazoezi na timu hiyo, wakati timu ikiingia kambini hoteli ya Bwawani
Jumatatu wiki hii jioni, hakutokea.
Hata
hivyo, Ahmed alisema siku ya pili yaani Jumanne ya Novemba 11 nyakati za jioni,
mmoja kati ya ndugu wa mchezaji huyo alikwenda Bwawani iliko kambi ya Zanzibar
Heroes, na kusema kuwa kiungo huyo amesafiri kwenda Dar es Salaam kutokana na
matatizo ya kifamilia.
“Yawezekana kama kweli Humud ana matatizo lakini wakati alikuwepo hapa angeweza kuja kambini na kutufahamisha badala ya kuondoka na baadae kutuma mtu. Huo si utaratibu,” alisema Machupa, baba wa mchezaji Adeyoum Saleh ambaye pia yumo katika kikosi hicho.
Alieleza kuwa, kukosekana kwa mchezaji huyo hakutaiathiri timu hiyo, kwani jana, wachezaji watatu walikuwa katika timu ya Taifa ya Tanzania, Khamis Mcha ‘Viali’, Waziri Salum na mlinda mlango Mwadini Ali, walitarajiwa kuwasili kambini baada ya kuachwa katika kikosi cha Stars kitakachoivaa Harambee Stars ya Kenya katika mechi ya kirafiki Jumanne ijayo.

No comments:
Post a Comment