Tajiri
huyo, Datta Phuge mwenye umri wa miaka 32, alitumia sawa na shilingi milioni 35
kutengeneza shati la dhahabu tupu ili kuwavutia wanawake wampende.
Tajiri huyo aliwaajiri masonara 15 wamtengenezee shati hilo ambalo anaamini litawafanya wanawake wampapatikie kutaka kuolewa naye.
Tajiri huyo wa mji wa Pimpri-Chinchwad, ambaye biashara yake kubwa ni kutoa mikopo kwa watu, aliwaajiri masonara hao ambao walifanya kazi kwa masaa 16 kwa siku kwa muda wa wiki mbili ili kulitengeneza shati hilo ambalo limekamilika kila kitu pamoja na vifungo vyake vya dhahabu.
"Najua kuwa mimi sio mwanaume mwenye kuvutia sana lakini nina uhakika hakuna mwanamke ambaye hatapagawishwa na shati langu", alitamba Datta.
"Shati la dhahabu lilikuwa miongoni mwa ndoto za vitu nilivyotaka kuwa navyo", aliendelea kutamba tajiri huyo kijana ambaye ana uhakika wanawake wataanza kumpigia misele kutaka kuolewa naye.

No comments:
Post a Comment