![]() |
| Kim Poulsen |
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Kim
Poulsen ameunda kikosi cha wachezaji 32 kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya
kimataifa dhidi ya Kenya (Harambee Stars) itakayochezwa Jumanne, Novemba 19
mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kikosi hicho kinajumuisha wachezaji 16 walioitwa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, na wengine 16 kutoka Future Taifa Stars. Awali kambi ya Future Taifa Stars iliyoanza Novemba 9 mwaka huu na kuvunjwa leo asubuhi ilikuwa na wachezaji 30.
Mabeki ni Aggrey Morris (Azam),
Ismail Gambo (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu Shooting),
Nadir Haroub (Yanga) na Said Moradi (Azam).
Viungo wakabaji ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam), Shomari Kapombe (AC Cannes, Ufaransa) na Vincent Barnabas anayechezea Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo, Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Jonas Mkude (Simba), Ramadhan Singano (Simba), Salum Abubakar (Azam) na William Lucian (Simba).
Viungo washambuliaji ni Faridi Musa (Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Mrisho Ngasa (Yanga), Mwingi Kazimoto (Markhiya, Qatar) na Simon Msuva (Yanga).
Washambuliaji ni Elias Maguli (Ruvu
Shooting), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC) na
Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).
Mnamo Novemba 19 Taifa Stars watacheza na Kenya, Harambee Stars, mchezo wa kirafiki Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam.
Future ilikuwaimeweka kambi hoteli ya Sapphire, wakati Stars ipo kambini Tansoma Hotel, zote maeneo ya Kariakoo, Dar es Salaam.
Future ilikuwaimeweka kambi hoteli ya Sapphire, wakati Stars ipo kambini Tansoma Hotel, zote maeneo ya Kariakoo, Dar es Salaam.

No comments:
Post a Comment