HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Saturday, 26 October 2013






EL CLASICO NI VITA KATI YA
Messi Vs Ronaldo
Neymar Vs Bale

>>LEO JUMAMOSI OKTOBA 26, NOU CAMP, SAA 1 USIKU

NI EL CLASICO ya 167 ndani ya Nou Camp Jijini Barcelona wakati FC Barcelona na Real Madrid zitakapocheza Mechi ya La Liga huku macho ya Washabiki safari hii yakiwakodolea ‘Wapya’ Gareth Bale na Neymar pamoja na kuwakazia wale wale wa zamani Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.

Ni Mechi pia itakayowakutanisha Mameneja wapya kwa Timu zote, Carlo Ancelotti toka Italy kwa Real Madrid na Gerardo Martino toka Argentina kwa Barcelona.
Wikiendi iliyopita, Barcelona walipoteza Pointi zao za kwanza kwenye La Liga baada ya kutoka Sare 0-0 na Osasuna na Real Madrid kushinda na kuwakaribia Barcelona ambao wako kileleni Pointi 3 mbele yao.

Mvuto kwa El Clasico hii ni Klabu zote mbili kuwa na Wachezaji wapya ambao wanaweza kucheza kwa mara ya kwanza kwenye mtanange wa aina hii kwa Barcelona kumchezesha Mchezaji mpya Neymar waliemnunua Msimu huu kutoka Santos ya Brazil na Real kumtumia Gareth Bale alievunja Dau la kununuliwa kwa Bei Ghali Duniani walipomnunua kwa Euro Milioni 100 kutoka Tottenham.
Lakini wakati Neymar akionyesha cheche zake kwenye Timu ya Barcelona, Bale amekuwa akikumbwa na Majeruhi yaliyomfanya acheze Mechi chache tu.

Kocha wa Real, Carlo Ancelotti, amedokeza kuwa Bale ataanza Mechi hii pamoja na Wachezaji wake wapya wengine Isco na Asier Illarramendi huku Cristiano Ronaldo akiongoa majeshi.
Nae, Gerardo Martino, amedokeza kuwa mashambulizi ya Kikosi chake yataongozwa na Lionel Messi na Neymar huku ukiwepo uwezekano wa Beki wao Mkongwe ambae pia ni Nahodha wao, Carles Puyol, kuanza Mechi hii baada ya kurudi tena dimbani akiwa nje akijiuguza Goti lake tangu Mwezi Machi.
+++++++++++++++++++++++
REKODI:
Uso kwa Uso:
-Real Madrid Wameshinda Mechi 90
-Barcelona Wameshinda Mechi 86
Mataji:
-Barcelona Vikombe 81
-Real Madrid Vikombe 76
+++++++++++++++++++++++

MECHI ZA MWISHO:
02-03-2013 Real Madrid: 2 FC Barcelona: 1 [La Liga]
26-02-2013 FC Barcelona: 1 Real Madrid: 3 [Copa Del Rey]
30-01-2013 Real Madrid: 1 FC Barcelona: 1 [Copa Del Rey]
07-10-2012 FC Barcelona: 2 Real Madrid: 2   [La Liga]
29-08-2012 Real Madrid  2  FC Barcelona 1 [Super Cup]
23-08-2012 FC Barcelona 3 Real Madrid 2 [Super Cup]
MSIMAMO-Timu za Juu:
NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
FC Barcelona
9
8
1
0
28
6
22
25
2
Atletico de Madrid
9
8
0
1
21
7
14
24
3
Real Madrid CF
9
7
1
1
19
9
10
22
4
Villarreal CF
9
5
2
2
15
9
6
17
5
Getafe CF
9
5
1
3
14
11
3
16
6
Athletic de Bilbao
9
5
1
3
15
13
2
16
7
RCD Espanyol
9
4
2
3
12
11
1
14

+++++++++++++++++++++++
LA LIGA-WAFUNGAJI BORA:
1 Diego Costa [Atletico Madrid] 10
1 Lionel Messi [Barcelona] 8
3 Cristiano Ronaldo [Real Madrid] 8
4 Pedro [Barcelona] 5
+++++++++++++++++++++++

No comments:

Post a Comment