Wabunge
wa CCM, Juma Nkamia (Chemba) na Hussein Bashe (Nzega Mjini), wameibana
Serikali wakitaka ishughulikie kupanda kwa bei ya mafuta na kuondoa kodi
ya tende ili kuwapunguzia mzigo wa gharama waislamu katika mwezi
mtukufu wa Ramadhani.
Hayo
yamejiri leo Mei 7, 2018 bungeni mjini Dodoma, wakati Nkamia
aliposimama kuomba mwongozo kuhusu mafuta na Bashe kutaka kuahirishwa
kwa shughuli za Bunge kwa dakika 30 ili kujadili suala la kodi ya tende
ili iondolewe kama ilivyo kwa nchi jirani.
Nkamia
alikuwa wa kwanza kuzungumza akisema, kubainisha kuwa katika baadhi ya
vyombo vya habari kuna taarifa za kuadimika kwa mafuta ya kula, “hali
hii inasababisha mafuta kupanda bei kwa haraka, Serikali inatoa kauli
gani ili kuwaondolewa wananchi hofu.”
Kwa
upande wake Bashe akitumia kanuni ya 69 ya kuahirisha shughuli za
Bunge, amesema, “mwezi wa Ramadhani unakaribia na kama alivyosema
Nkamia, bei ya mafuta imepanda, sukari imepanda, lakini nchi
zinazotuzunguka zimefuta kodi za tende.”
Akijibu
mwongozo huo, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage
amesema tatizo lililojitokeza ni suala la kodi kwani kwa sasa Taifa
lina hifadhi ya mafuta ghafi tani 40,000 na meli zilizopo nje zina tani
50,000.
“Jumla
zilizoko nje na ndani zina tani 90,000. Kinachoweka tatizo ni kodi kwa
sheria tulizopitisha Tanzania, tunatoza kodi (meli kutoka nje ya nchi)
asilimia 10 kwa mafuta ghafi,” amesema.
“Ila
kwa vipimo vinaonyesha si mafuta ghafi ni mafuta masafi hivyo wanataka
kutoza asilimia 25 na hapo ndipo kuna tatizo la hadi kufikia leo au
kesho tutatoa majibu ya tulipofikia.”
Kuhusu
hoja ya tende iliyoulizwa na Bashe, Waziri Mwijage amesema, “ni suala
la kwenda kuzungumza na waziri wa fedha, tutalipeleka kuweza kumshawishi
ili Bunge na nchi ichume thamani.”
Naye,
Waziri wa Kilimo, Dk Charles Tizeba amesema suala la mbegu za pamba
kutumika kukamulia mafuta zilipatikana mwaka jana zaidi ya laki moja.
“Suala
la mafuta yanayotokana na pamba, kwa uhakika hayakutarajia kuwa mengi,
sasa Serikali inachokifanya inaagiza kutoka nje, niseme tu suala la
mafuta linafahamika na Serikali inalifanyia kazi na haitapanda bei sana
kama mbunge (Nkamia) alivyoonyesha wasiwasi,” amesema Tizeba.
No comments:
Post a Comment