Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina wakati wa sherehe za ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km 251 |
Rais Magufuli amesema hayo leo April 27, 2018 wakati akifungua barabara ya lami kutoka Dodoma hadi Babati, Manyara yenye urefu wa kilometa 251 ambayo imegharimu Tsh. Bilioni 378.
“Siwezi kuhangaika kutafuta fedha za kujenga barabara, kununua ndege, viwanja, alafu bado nitafute na fedha za kuwanunulia chakula cha bure. Nasema, hakuna chakula cha bure, ambaye hatalima, atakufa njaa,” amesema Rais Magufuli.
“Mvua imeenyeesha miezi yote halafu ije itokee mwezi wa ngapi mseme tunaomba chakula kuna njaa tutakufa nitasema tu kufa. Nawaambia Watanzania wote kuanzia Kongwa mpaka Chato hakuna chakula kitakachogaiwa mwaka huu,” amesisitiza.
Hivi karibuni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema hali ya uzalishaji wa mazao ya chakula nchini imeimarika na kufikia tani milioni 15.9 kwa msimu wa kuanzia mwaka 2016 hadi 2018 sawa na kuwa na ziada ya tani milioni 2.6 za chakula.
No comments:
Post a Comment