HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Monday, 11 December 2017

MTOTO WA MIAKA 6 ALIWA NA FISI MKOANI GEITA.


MTOTO mwenye umri wa miaka sita Joseph Simon [6] mkazi wa kijiji cha Buzanaki, Kata ya  Nyamarimbe wilaya na mkoa wa  Geita ameuawa na fisi na kisha kuliwa baadhi ya viungo vya mwili wake kabla ya familia kwa kushirikiana na wanakijiji kuokota mabaki ya mwili wake.

Wanakijiji wakishirikiana na familia husika walifanikiwa  kuokota mabaki ya mwili wa mtoto huyo yakiwamo utumbo na kipande cha mfupa wa ambavyo vilizikwa kwa heshima kijijini Buzanaki na tayari fisi saba wameuawa katika nyakati tofauti katika oporesheni ya kuwasaka.

Ofisa wanyamapori wa Halmashauri ya wilaya ya Geita, Msese Kabulizina, alisema tukio hilo lilitokea Desemba 2, mwaka huu zikiwa ni siku tatu tangu wakazi wengine wa Kijiji cha Idoselo Kata ya Luezela wilayani Geita nao kujeruhiwa na fisi kisha kulazwa katika Hospitali ya Rufani ya mkoa wa Geita.

Tukio hilo lilitokea usiku wa Desemba 2,wakati akitoka kuchuma embe zikiwa ni siku mbili tu baada ya wakazi wengine watatu wakazi wa kijiji tofauti cha Idosero Kata ya Luezera  kujeruhiwa na fisi.

Walwa aliongeza kuwa tukio la kujeruhiwa watu watatu lilitokea usiku wa  kuamkia Novemba 29 usiku baada ya kundi la fisi wanaodaiwa kuwa zaidi ya wanne kuvamia nyumbani  kwa mzee  Magadula kisha kuishambulia familia hiyo kabla majirani kufika kutoa msaada na wao kujeruhiwa.

Aliongeza  baada ya fisi hao kuvamia ndipo familia hiyo ilipopiga makelele kuomba msaada na majirani waliofika kwanza walikuwa ni Kulwa Jamoka na mwanaye  Yohana Kulwa ambao katika kutoa msaada nao walijikuta wakijeruhiwa.

Hata hivyo, wakati makelele yakiendelea huku fisi nao  wakishambulia wao na mbuzi nakumtafuna kabla ya umati wa  wanakijiji kuongezeka na kuanza msako  ambapo hadi  Jumamosi walikuwa wameuawa fisi saba  katika matukio tofauti kwa kusaidiana Idara ya Askari  wanyamapori Halmashauri ya wilaya ya Geita.

No comments:

Post a Comment