Serikali
amewaagiza wote waliohitimu kidato cha sita Mei mwaka huu na ambao hawajajiunga
na vyuo vya elimu ya juu, wakaripoti katika kambi za Jeshi la Kujenga Taifa
(JKT) Desemba Mosi, mwaka huu.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga
Taifa, Dk Hussein Mwinyi (pichani kulia) ametoa agizo hilo mjini Dodoma alipozungumza na
waandishi wa habari katika Ukumbi wa Habari wa Bunge.
Dk Mwinyi alisema Mei na Juni mwaka
huu, JKT iliwafanyia usaili vijana wa kujiunga na JKT kwa kujitolea. Alisema
usaili huo ulifanyika kwa kushirikiana na kamati za ulinzi za wilaya na mikoa.
“Wizara ya Ulinzi na JKT inapenda
kuwatangazia vijana wote waliosailiwa Juni mwaka huu, kujiunga na JKT kwa
kujitolea, waripoti kwenye kambi walizopangiwa ifikapo Desemba Mosi mwaka huu
kwa nauli zao,” amesema Dk Mwinyi.
Dk Mwinyi amesema mafunzo hayo ni ya
miezi mitatu kwa mafunzo yenye utaratibu wa kawaida na miaka miwili kwa wa
kujitolea.
Ili kufanikisha hilo, Wizara
ilimuagiza Mkuu wa JKT kufufua kambi ya Makuyuni JKT iwe miongoni mwa kambi
kuanzia Desemba mwaka huu.Aliagiza kambi za Luwa na Milundikwa za mkoani Rukwa,
zirejeshwe kwa shughuli za JKT za kilimo na ufugaji.
Dk Mwinyi alimuagiza Mkuu huyo wa
JKT pia kambi ya Mpwapwa irejeshwe kwa ajili ya kuendesha mafunzo ya kilimo na
ufugaji ndani ya JKT.
No comments:
Post a Comment