WANAFUNZI
shule ya msingi ya Machemba Wilayani Muheza mkoani hapa wamelazimika kusomea
chini ya mti na wengine kukaa chini kufuatia upungufu wa vyumba vya madarasa na
madawati hali inayopelekea kukatisha masomo
wakati wa mvua.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwalimu mkuu wa
shule hiyo, John Ngadallah, alisema kwa muda mrefu wanafunzi wamekuwa
wakilazimika kusomea chini ya miti kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa na
madawati.
Amesema shule hiyo ina wanafunzi 354 ambapo wanafunzi 122
wanasomea chini ya mti huku shule hiyo ikiwa na vyumba vinne vya madarasa ambapo
wakati wa mvua na hulazimika kusitisha
masomo kwa muda.
Mwalimu huyo amewataka wadau wa elimu, mashirika na watu
binafsi wenye uwezo kuisaidia shule hiyo ili kuondokana na kero ya wananfunzi
kusoma chini ya mti na kuweza kuwandaa
vijana kielimu na kuwa msaada kwa taifa.
“Kama mulivyoona hapa wanafunzi wanasomea
chini ya miti ni kutokana na uhaba wa vyumba vya madarsa na madawati, jambo
hili linatuumiza kichwa sana kuweza kulimaliza” alisema Ngadallah na kuongeza
“Tumepeleka maombi kwa wadau wa elimu mbalimbali lakini muitikio bado ila nina
imani kupitia kwenu kilio chetu kitasikika” alisema
Naye Mwenyekiti wa Serikali ya kitongoji, Said Juma, alisema
ili kutatua changamoto zinazoikabili shule hiyo wamelazimika kufanya mkutano wa
kijiji na kukubaliana kila kaya kuchangia matofali matatu ili kuanza ujenzi wa
vyumba vya madarasa.
“Changamoto ni nyingi shuleni pale
lakini kwanza tumeadhimia kuanza na mambo muhimu mawili kwa matatu, kuongeza
vyumba vya madarasa na madawati pamoja na matundu ya vyoo” alisema Juma
Amesema ujenzi huo utaambatana na ujenzi wa matundu ya vyoo
ambapo shule sasa ina matundu mawili ya vyoo moja kwa wanafunzi wa kike na
jengine kwa wanafunzi wa kiume.
Mwenyekiti huyo aliwataka wananchi
kutoa ushirikiano na kujitolea kwa moyo mmoja ili kero hiyo iweze kumalizwa na
kuwawezesha wanafunzi kusoma wakiwa madarasani na wamekalia madawati.
IMETOLEWA TANGA KUMEKUCHA BLOG
No comments:
Post a Comment