Arsenal
wapo tayari kutoa pauni milioni 13.4 kumsajili msambuliaji wa Celta Vigo,
Nolito (Mundo Deportivo),
Manchester
United wameanza mazungumzo na mshambuliaji wa Atletico Madrid Saul Niguez (pichani) (Daily Mirror),
mshambuliaji
wa Tottenham, Harry Kane amesema Spurs wana mustakbali mzuri na anataka kusalia
katika klabu hiyo, licha ya kuhusishwa na kuhamia Real Madrid mwisho wa msimu (Sun),
Spurs
pia watapambana na Galatasaray ya Uturuki kutaka kumsajili Loic Remy kutoka Chelsea (Daily Express),
mshambuliaji
wa West Brom, Saido Berahino anataka kujiunga na Tottenham katika dirisha hili
la usajili na atakataa dau kutoka klabu nyingine yoyote (Sun),
hata
hivyo Liverpool watajaribu kumshawishi Berahino kwenda Anfield kuchukua nafasi
ya Daniel Sturridge (Daily Express),
meneja
wa Aston, Villa Remi Garde anataka kukibadili kikosi hicho kwa kwanza kuwaondoa
nahodha Gabriel Agbonlahor na winga Charles Nzogbia (Times),
meneja
wa Borussia Dortmund Thomas Tuchel amesema Neven Subotic anayesakwa na
Liverpool haendi popote mwezi huu (Liverpool
Echo),
beki
wa Leicester Ben Chilwell anasakwa na Arsenal na Liverpool (Telegraph),
mshambuliaji
wa zamani wa Arsenal Niklas Bendtner huenda akaondoka Wolfsburg na kwenda
Newcastle United (Bild),
kiungo
wa Lazio, Filipe Anderson anasema hafahamu kama atakuwepo bado Italia mwisho wa
mwezi Januari (Daily Star),
licha
ya kumsajili kiungo kutoka Senegal, Henri Saivet, meneja wa Newcastle, Steve
McClaren anamtaka mmiliki wa klabu hiyo, Mike Ashley kuongeza wachezaji zaidi
ili wasishuke daraja (Guardian),
Newcastle
wametoa pauni milioni 10 kumtaka kiungo wa Swansea, Jonjo Shelvey, lakini
huenda wakalazimika kulipa pauni milioni 12 kumpata (Telegraph),
Chelsea
wanamfuatilia mshambuliaji wa AC Milan, Carlos Bacca, ambaye amepachika mabao
manane msimu huu (Daily Mail),
Southampton
wataongeza dau lao la pauni milioni 12.2 kutaka kumsajili kiungo Stefano
Sturaro kutoka Juventus (Daily Mirror).
No comments:
Post a Comment