Uongozi wa Serikali ya Mtaa Mtaa wa Sumbawanga chini ya
Mw/kiti wake Mr Kiswabi jana Des 19 ulifanya mkutano na wakaazi wa mtaa huo
kujadili mipango ya maendeleo na changamoto mbalimbali zinazo kabili wananchi
hao.
Agenda kuu za mkutano
huo zilikuwa ni kero kati ya Wakulima, Wafugaji na wasio wafugaji, Usafi wa
mazingira, Ulinzi na Usalama, miundo mbinu ya barabara na taarifa ya Mapato na
Matumizi.
Akizungumza kwenye
mkutano huo M/kiti wa Serikali ya ya Mtaa Mr Kiswabi alibainisha kuwa
Halmashauri ya jiji la Tanga imetoa kipindi cha miaka mitano kwa wafugaji wote
kuondoa mifugo yao ndani ya maeneo ya makazi ya watu na kwa sasa mfugaji
atatozwa faini ya sh 50000/= iwapo atashindwa kudhibiti mifugo yake. Hata hivyo
mmoja wa wakazi wa mtaa huo aliyetambilika kwa jina la Mama Simkoko
alipendekeza iongezwe faini y ash 20000 kwa uharibifu unaosababishwa na mifugo
wazo ambalo lilikubalika na mkutano huo.
Kuhusu Ulinzi na
usalama kamati ya ulinzi ya mtaa huo imetoa angalizo kjwa kila mkaazi kuwa
mlinzi wa mwenzake na kutoa ripoti ya matukio ya uvunjifu wa sherika kwa
haraka. Kuhusu usafi wa mazingira Mkiti wa Mtaa huo amewataka wananchi
kujitokeza kwa wingi kila inapogigwa mbiu ya msaragambo wa usafi kwenye mtaa
huo.
Katika hatua nyingine
baadhi ya wananchi walieleza kusikitishwa kwao na hatua ya Serikali ya Mtaa huo
kutoa posho y ash 10,000/= kwa wajumbe wa serikali hiyo bila ridhaa ya
Wananchi.
Mmoja wa wananchi hao
aliyetambulika kwa jina maarufula Bw Tiotimo ameitaka Serikali ya mtaa huo
chini ya Mw/kiti wake iweke utaratibu wa kuomba ridhaa kwa wananchi kama
itahitaji kutoa fedha za Serikali hiyo kwa matumizi mbalimbali, huku akihoji
kwanini akidi ya wajumbe itokee upande mmoja pekee.
Akijibu hoja hizo
M/kiti wa Mtaa huo amesema fedha hiyo ilitoka baada ya maridhiano ya wajumbe na
taariwa ilitolewa kwenye kikao kingine huku akiwataka wananchi kujitokeza
kwenye mikutano kama hiyo ili kufahamu nini kinaendelea.
No comments:
Post a Comment