Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetangaza
kufuta hati miliki ya shamba la mkonge la Kikwetu mkoani Lindi baada ya mmiliki
wake kampuni ya Amboni Estates Ltd kushindwa kuliendeleza hadi sasa.
Kwa mujibu wa Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa wakati akizungumza na wakazi wa Lindi alisema serikali
imechukua hatua hiyo kufuatia kushindwa kuliendeleza ambapo shamba
hilo litakuwa kuwa chini ya serikali.
Aidha, Shamba hilo linalodaiwa
kupewa hati ya umiliki wa miaka 99 na baadaye kampuni ya Tasco kabla ya
kuchukuliwa na Mohamed Enterprieses Tanzania Ltd lilikuwa likizalisha mkonge
kwa ajili ya kutengeneza magunia.
Katika mkutano huo Majaliwa
alisema tayari shamba hilo lipo huru na kampuni ya BSG ipo huru kujenga mitambo
itakayotumika kusafishia gesi asilia kwenye eneo hilo.
Akizungumzia uendelezwaji wa
kiwanda cha kuzalisha saruji cha Meis ambacho ujenzi wake umesimama kwa muda
kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo za kisiasa, Majaliwa alisema kazi hiyo
inatarajiwa kuanza tena muda mfupi ujao baada ya kupatikana kwa wataalam.
Kwa upande mwingine Majaliwa alisema
kujengwa kwa viwanda ndani ya mji huo, kutasaidia kupunguza tatizo la
upatikanaji wa ajira kwa wananchi wa Mkoa wa Lindi na vitongoji vyake.
No comments:
Post a Comment