Jumanne Usiku Robo
Fainali za UEFA CHAMPIONZ LIGI zitaanza kwa Mechi mbili na moja ikiwa huko Jiji
la Madrid, Spain ndani ya Estadio Vicente Calderon wakati Atletico Madrid
watakapokuwa Wenyeji wa Mahasimu wao Real Madrid.
Mechi hii, Dabi ya Madrid, maarufu kama
El Derbi Madrileño, ni Marudio ya Fainali ya Msimu uliopita ya UEFA CHAMPIONZ
LIGI ambayo Real Madrid waliinyuka Atletico Madrid Bao 4-1 na kutwaa Ubingwa wa
Ulaya kwa mara ya 10.
Mechi nyingine ya Jumanne Usiku itachezwa
huko Jiji la Turin Nchini Italy wakati Wenyeji Juventus watakapoivaa AS Monaco
ya France.
PATA TATHMINI YA MECHI.
Kila Timu itaingia kwenye Mechi hii
ikidhamiria kisasi.
Kwa Atletico, kisasi chao ni kile cha
kufungwa na Real kwenye Fainali ya Mashindano haya huko Lisbon Msimu uliopita
na kwa Real ni kubondwa mara 4 na Sare 2 na Atletico tangu Fainali hiyo.
Vipigo kwa Real ni pamoja na kutupwa
nje ya Spain Supercup na Copa del Rey.
Katika pambano lao la mwisho Mwezi
Februari, kwenye Mechi ya La Liga, Atletico iliitwanga Real 4-0 ikiwa ndio
ushindi wao mkubwa dhidi ya Wapinzani wao wakubwa katika Miaka 28.
Hilo limemfanya Kocha wa Real, Carlo
Ancelotti, aseme: "Matokeo ya mwisho na Atletico ndio yanatupa motisha
sisi!"
Lakini, tofauti na Mechi zilizopita
Msimu huu, safari hii Real watatinga kwa maadui zao Vicente Calderon wakiwa na
Kikosi kamili kwa mara ya kwanza katika Miezi Mitano.
James Rodriguez na Toni Kroos,
ambao waliikosa Mechi ya La Liga ya Jumamosi walipoifunga Eibar 3-0 baada
ya kuwa Kifungoni, wanarejea dimbani.
Nao Atletico wana habari njema ya
kurejea dimbani baada ya kuzikosa Mechi mbili akijiuguza Enka kwa Straika wao
Mario Mandzukic ambae tangu ahamie Atletico akitoka Bayern Munich
mwanzoni mwa Msimu amepachika Bao 20 zikiwemo Bao 2 katika Gemu mbili dhidi ya
Real Uwanjani Vicente Calderon.
Jumatano pia zipo mechi mbili nyingine
za Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI kati ya PSG na Barcelona huko Mjini
Paris na nyingine itachezwa huko Ureno kati ya FC Porto na Bayern Munich.
VIKOSI VINATARAJIWA:
Atletico
Madrid: Oblak; Juanfran,
Miranda, Godín, Gámez; Arda Turan, Tiago, Suárez, Koke; Griezmann, Mandžukić.
Real Madrid: Casillas; Carvajal, Pepe, Ramos, Marcelo; Kroos, Modrić,
James; Bale, Benzema, Ronaldo.
REFA: Milorad Mažić (Serbia)
RATIBA
Robo Fainali-Mechi za Kwanza
**Mechi zote kuanza Saa 3 Dakika 45
Usiku, Saa za Bongo
Jumanne Aprili 14
Atlético Madrid v Real Madrid
Refa: Milorad Mažić (Serbia) – Uwanja:
Estadio Vicente Calderón, Madrid, Spain
Juventus v AS Monaco
Refa: Pavel Královec (Czech Republic) –
Uwanja: Juventus Stadium, Turin, Italy
Jumatano Aprili 15
Paris Saint-Germain v Barcelona
Refa: Bado kujulishwa– Uwanja: Parc des
Princes, Paris, France
FC Porto v Bayern Munich
Refa: Bado kujulishwa – Uwanja: Estádio
do Dragão, Porto, Portugal

No comments:
Post a Comment