HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Thursday, 5 March 2015

WAZIRI MKUU AZINDUA TAARIFA YA MWAKA WA KWANZA WA UTEKELEZAJI WA MFUMO WA "BRN"


WAZIRI MKUU Mh.Mizengo Pinda

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema kuwa Serikali itahakikisha kuwa
sekta na miradi inayotambuliwa na kuingizwa kwenye Mfumo wa Tekeleza
kwa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now au BRN) ni ile yenye manufaa
makubwa nay a haraka kwa wananchi walio wengi.


Ametoa kauli hiyo leo mchana (Alhamisi, Machi 5, 2015) wakati
akizungumza wa wadau mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa taarifa ya
mwaka wa kwanza ya utekelezaji wa Mfumo wa Tekeleza kwa Matokeo
Makubwa Sasa kwenye uliofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini
Dar es Salaam.

“Vigezo hivi ndivyo vilivyotumika kutambua sekta sita za mwanzo ambazo
ni kilimo, elimu, nishati, uchukuzi, utafutaji rasilmali fedha na maji
ambazo leo ndiyo tunapokea taarifa ya utekelezaji wake kwa mwaka wa
kwanza,” alisema.

Alisema vigezo hivyo pia vilitumika kuchagua mazingira ya biasharana
huduma za afya kuziingiza kwenye utaratibu wa BRN. “Serikali inaamini
kwamba kuimarika kwa mazingira ya biashara, hasa biashara ndogondogo,
kutatoa fursa za watu wengi zaidi kujiajiri na kuajiri na kuajiri
wengine,” aliongeza.

Alitoa wito kwa watendaji wote kujifunza na kuutumia mfumo huo ili
waweze kufikia malengo waliyojiwejkea kwa  haraka zaid. “Mambo matatu
yanayoupa mfumo huu uwezo mkubwa zaidi ni kupanga kipaumbele; kuwa na
nidhamu na uwazi; na haya mambo yako ndani ya uwezo wa kila Mmoja wetu
,” alisema.
Alisema Serkali itaendelea kuchukulia utekelezaji wa mfumo wa Tekeleza
kwa Matokeo Makubwa Sasa kama jambo la kipaumbele katika kutekeleza
majukumu yake.
“Haitoshi kwamba tumepata mafanikio haya katika mwaka Mmoja. Ni lazima
sasa tuazimie sote kuchukua kanuni hizi na kuzitumia katika kila eneo
la maisha yetu. Hiyo ndiyo njia pekee ya kuhakikisha tumetoa mchango
kamili kwa Taifa letu kufikia malengo yaliyoainishwa kwenye Dira ya
Taifa ta Maendeleo hadi mwaka 2015,” alisema.

No comments:

Post a Comment