Mganga
wa Jadi Rashid Omar Ibrahim (40) wa Chamboni Wilaya ya Micheweni amepelekwa
rumande kwa kipindi cha siku kumi na mahakama ya Wilaya ya Wete baada ya
kufikishwa mahakamabni akikabiliwa na tuhuma za ubakaji.
Imedaiwa
mahakamani hapo na Mwendesha mashitaka Mkaguzi wa Polisi Fakih Yussuf
mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Rashid Machano Magendo kuwa mtuhumiwa huyo
ametenda kosa hilo februari 20 mwaka huu .
Ameeleza
kwamba siku ya tukio huko Kitambuu Mchangamdogo Wilaya ya Wete , mtuhumiwa huyo
alimwingilia mwanamke mwenye umri wa miaka 40 na kumsababishia maumivu makali .
Mwendesha
mashtaka wa Polisi amezidi kufahamisha kwamba kosa hilo ni kinyume na kifungu
cha 125 (I) ,(2) na kifungu cha 126 (I) cha Sheria namba 6 ya mwaka 2004 sharia
za Zanzibar .
Baada
ya kusomewa shitaka lake mtuhumiwa huyo hakutakiwa kujibu loloteb kutokana na
mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusilikiza kesi za aina hiyo ambapo
amepelekwa rumande hadi tarehe 9 mwezi huu kesi itakapokuja kutajwa tena katika
mahakama ya Mkoa.
No comments:
Post a Comment