HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Tuesday, 31 March 2015

BONDIA FRANCIS CHEKA KUPANDA ULINGONI KWA MARA YA KWANZA MWEZI MEI MWAKA HUU.



HUKO MOROGORO.BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini Francis Cheka (SMG) anatarajia kupanda ulingoni kwa mara ya kwanza mwaka huu kuzipiga na mmoja wa mabondia wa kimataifa kutoka Marekani kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Cheka anatarajia kupanda ulingoni kuvaana na bondia mmojawapo wa kimataifa kati ya Pascal Bruno wa Marekani ama Alanbek Kozaed wa Uingereza na limepangwa kufanyika Mei 30.

Promota wa bondia huyo Kaike Siraji alisema hayo jana mjini hapa wakati akizun gumza na waandishi wa habari baada ya bondia huyo kusaini mkataba wa pambano hilo.

Kabla ya kuzungumzia pambano hilo Promota huyo alisema kuwa licha ya Cheka kutumikia kifungo cha nje, masharti aliyopewa ni kufanya kazi saa nne kwa siku za kazi na kuwa na mapunziko kwa Jumamosi na Jumapili.

Hivyo kulingana na utaratibu wa kazi za kuitumikia jamii zilizo katika kifungo chake cha nje kumempa fursa ya kuzitumia saa zinazosalia baada ya kuitumikia jamii kujihusisha na kazi binafsi za kumuingizia kipato.
Kutokana na fursa hiyo, Promota huyo alisema pambano lililoandaliwa linasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa ngumi ndani na nje ya mkoa wa Morogoro kufuatia bondia huyo kukaa muda mrefu bila pambano.

Naye Cheka alitumia fursa hiyo kuwataka mashabiki wake kusahau mambo yaliyopita na wagange yajayo na kwamba yaliyotokea ni mambo ya kijamii ambayo mwanadamu yeyote yanaweza kumtokea.
Pamoja na kuzungumzia pambano hilo,Cheka alimpongeza bondia mwenzake, Mohammed Matumla, baada ya kuibuka na ushindi kwa kumpiga kwa pointi bondia Wang Xing Hua kutoka China.

Cheka alihukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Mkoa wa Morogoro kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kutiwa hatiani kwa kumpiga Meneja wake wa baa Bahati Kibanda kabla ya Machi 17, mwaka huu kubadilishiwa adhabu na kutumikia kifungo cha nje.

Kifungo hicho cha nje alianza kukitumikia baada ya Maofisa Huduma kwa Jamii kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ,kupitia na kufuata taratibu kwa makosa aliyotenda ili kuhakikisha anatumikia adhabu mbadala kwa jamii aliyoikosea.

No comments:

Post a Comment