TIMU ya
Mtibwa Sugar, imeendeleza wimbi la ushindi na kubaki kuwa moja kati ya timu 2
ambazo hazijafungwa katika Ligi Kuu, baada ya kuifunga Mbeya City ya Hapa kwa
mabao 2-0 katika pambano kali kwenye Uwanja wa Sokoine hapo jana.
Kocha
Mtibwa Sugar “MECKY MEXIME”
|
Ushindi
huo umeiweka juu zaidi timu ya Mtibwa Sugar kwa toafuti ya pointi tatu, baada
ya kuifanya kufikisha pointi 13, huku ikiziacha Yanga na Azam FC zikibanana
katika nafasi ya pili kwa kuwa na pointi 10 baada ya mechi tano tano kwa kila
kikosi tangu kuanza kwa msimu huu wa 2014/15.
Bao la
kwanza la Mtibwa Sugar lilifungwa dakika ya 20 na nyota wake Ame Ally,
akiunganisha kona iliyopigwa na beki wa kushoto wa zamani wa Yanga anayekipiga
na ‘Wakata Miwa’ hao kwa sasa, David Luhende. Baada ya bao, Mtibwa waliendelea
kuishambulia Mbeya City na nusura wapate bao la pili dakika ya 31 kupitia Ally
Shariff. hadi mapumziko, matokeo yalikuwa wageni kuongoza mechi kwa bao hilo
1-0 dhidi ya wenyeji wao ambao msimu huu unaonekana kuwa mgumu kwao.
Kipindi
cha pili kilianza kwa kasi ya aina yake Mbeya City wakipania kusawazisha bao,
ambako walianza na badiliko la kumtoa Themi Felix na nafasi yake kuchukuliwa na
Peter Malyanzi, ambaye nusura aipatie timu yake bao la kusawazisha, lakini
shuti lake dakika ya 53 lilidakwa na kipa wa Mtibwa Said Mohammed.
Dakika
ya 76, Mtibwa wakajihakikishia ushindi muhimu, kutokana na bao maridadi la
Andrew Vicent, alilofunga baada ya kuwalaamba chenga mabeki wa Mbeya City na
kufumua shuti kali na kumshinda kipa David Burhani.
Dakika
moja kabla ya filimbi ya mwisho ya mwamuzi Hashimu Abdallah wa Dar es Salaam,
Mtibwa nusura wapate bao la tatu, lakini shuti la adhabu ndogo nje ya boksi,
iliyotokana na Vicent kuchezewa rafu, kupaa nje ya lango. Hadi mwisho, Mtibwa
Sugar 2 Mbeya City 0.Timuu nyingine ambayo haijapoteza mchezo mpaka sasa ni
Simba Sport Club.
Vikosi
katika pambano hilo vilipangwa hivi, Mbeya
City: David Burhani, Kenny Ally, Hassan Mwasapili, Deogratius Julius,
Yohana Morris, Yusuph Abdallah, Deus Kaseke, Steven Mazanda, Paul Nonga, Saad
Kipanga na Themi Felix.
Mtibwa
Sugar: Mtibwa Sugar, Said Mohammed,
David Luhende, Salim Mbonde, Andrew Vicent, Shabani Nditi, Mussa Hassan
‘Mgosi’, Mohammed Ibrahim, Ame Ally, Mussa Nampaka na Ally Shariff.
Dakika 90 za mchezo
wa ligi kuu ya Tanzania Bara kati ya Yanga ya jijini Dar es salaam na Stand
United, zilimalizika huku Yanga wakiibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0, bao la
kwanza likifungwa na Jelson Jaja la pili na la tatu yakifungwa na Jerson Tegete
katika mchezo uliopigwa Oct 25 mwaka huu.
Wakati Yanga wakishinda mabao 3-0 Watani wa Simba wao wameendeleza rekodi yao ya kutoka sare, ambapo hadi sasa tayari wameshacheza mechi tano na wakiwa na Pointi tano, huku katika mchezo wa leo wakitoka sare ya bao 1-1 na Tanzania Prisons huko jijini Mbeya.
Wakati Yanga wakishinda mabao 3-0 Watani wa Simba wao wameendeleza rekodi yao ya kutoka sare, ambapo hadi sasa tayari wameshacheza mechi tano na wakiwa na Pointi tano, huku katika mchezo wa leo wakitoka sare ya bao 1-1 na Tanzania Prisons huko jijini Mbeya.
MATOKEO- Mechi
zilizopita:
Jumamosi Oktoba 25
Stand United 0 Yanga 3
Azam FC 0 JKT Ruvu 1
Prisons 1 Simba 1
Kagera Sugar 1 Coastal Union 1
Ruvu Shooting 1 Polisi Moro 0
Ndanda FC 0 Mgambo JKT 1
LIGI KUU VODACOM
MSIMAMO:
NA
|
TIMU
|
P
|
W
|
D
|
L
|
F
|
A
|
GD
|
PTS
|
1
|
Mtibwa Sugar
|
5
|
4
|
1
|
0
|
8
|
1
|
7
|
13
|
2
|
Azam FC
|
5
|
3
|
1
|
1
|
6
|
2
|
4
|
10
|
3
|
Yanga
|
5
|
3
|
1
|
1
|
7
|
4
|
3
|
10
|
4
|
Coastal Union
|
5
|
2
|
2
|
1
|
6
|
4
|
0
|
8
|
5
|
JKT Ruvu
|
5
|
2
|
1
|
2
|
4
|
5
|
-1
|
7
|
6
|
Ruvu Shooting
|
5
|
2
|
1
|
2
|
4
|
5
|
-1
|
7
|
7
|
Kagera Sugar
|
5
|
1
|
3
|
1
|
3
|
2
|
1
|
6
|
8
|
Mgambo JKT
|
5
|
2
|
0
|
3
|
2
|
4
|
-2
|
6
|
9
|
Tanzania Prisons
|
5
|
1
|
2
|
2
|
5
|
5
|
0
|
5
|
10
|
Simba
|
5
|
0
|
5
|
0
|
5
|
5
|
0
|
5
|
11
|
Mbeya City
|
5
|
1
|
2
|
2
|
1
|
2
|
-1
|
5
|
12
|
Stand United
|
5
|
1
|
2
|
2
|
3
|
8
|
-5
|
5
|
13
|
Ndanda FC
|
5
|
1
|
0
|
4
|
7
|
10
|
-3
|
3
|
14
|
Polisi Moro
|
5
|
1
|
2
|
2
|
3
|
6
|
-3
|
3
|
No comments:
Post a Comment