Hata hivyo, Ambroce alisema mahakamani hapo anashangaa kushtakiwa na watu ambao hawajui lakini Hakimu Devotha Msofe alimtaka anyamaze kwani kesi hiyo haijaanza kusikilizwa.
Akiwasomea mashtaka hayo mbele ya Hakimu Msofe, Wakili wa Serikali Felix Kwetukia aliwataja washtakiwa wengine kuwa ni Abashar Omar (24), Hassan Omari (40), Abdulrahman Hassan(41), Baraka Bilango (40), Niganya Niganya (28), Morris Muzi (44), Ramadhan Waziri (28), Yusuph Huta (30), Kassim Idrisa (34), Said Michael (42), Jaffari Lema (38) na Abdul Mohammed (30).
Kwetukia alidai mahakamani hapo kuwa washtakiwa hao kwa pamoja Mei 5, mwaka 2013 katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Olasiti jijini Arusha walimuua Patricia Joachim, Regina Loning’o na James Gabriel Kessy.
Pia washtakiwa hao wanatuhumiwa kwa makosa 18 ya kujaribu ya kuwaua Neema David, Herbert Njau, Regina David, Consesa Mbaga, Amarin Pius, Atanasia Reginald, Elizabeth Isdory, Alphonce Nyakundi, Joyce Yohana na Genesi Pius.
Wengine waliojaribu kuwaua ni Teofrida Innocent, Gabriel Godfrey, Manswet Siril Kessy, Editha Ndowo, LovenessNelson, Debora Joachim, Mathias Kiya na Restituta Alex Matemu.
Baada ya kusomewa mashtaka yao, Hakimu Msofe aliwaambia washtakiwa hawaruhusiwi kujibu chochote na kuwapa nakala ya hati ya mashtaka lakini mshtakiwa Ambroce alinyoosha kidole na kuruhusiwa kuongea ndipo aliposema “Mheshimiwa Hakimu mimi nashangaa kuona naunganishwa na washtakiwa ambao hata siwafahamu.”
Mara baada ya kusema hivyo Hakimu alimtaka mshitakiwa huyo anyamaze maana kesi hiyo inatajwa tu haijasomwa ikisomwa ndipo ataweza kuuliza maswali hayo ila kwa sasa hakuna chochote kinachoendelea. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Agosti 29, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment