RYAN
GIGGS ameteuliwa kuwa Meneja wa Muda mpya wa Manchester United baada David
Moyes kutimuliwa hii Leo.
Moyes,
ambae alishika wadhifa Julai Mosi Mwaka Jana, amefukuzwa kazi kufuatia Msimu
mbovu wa Mabingwa hao wa England ambao wameshindwa kutetea Taji lao na pia
kushindwa kufuzu kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao kwa vile watakuwa nje
ya 4 Bora na hii ni mara ya kwanza tangu Mwaka 1991 kwa Man United kushindwa
kumaliza ndani ya 3 Bora.
Ryan
Giggs, mwenye Miaka 40, ni Kocha-Mchezaji wa Man United Klabu ambayo alianza
nayo tangu yuko mdogo.
Mechi
ya kwanza chini ya Giggs itakuwa ni Jumamosi Aprili 26 Uwanjani Old Trafford
wakati Man United itakapocheza na Norwich City kwenye Mechi ya Ligi Kuu
England.
Uteuzi
wa Giggs kama Meneja umepokewa vizuri na Wachezaji wa zamani wa Man United kina
Dwight Yorke na David May.
Wakati
May alisema Giggs ni chaguo zuri sana kwa Man United kulifanya, Dwight Yorke
alisema yeye angemchagua Giggs tangu mwanzo alipostaafu Sir Alex Ferguson.
Yorke
amesema: “Yeye amekuwepo Klabuni kwa Miaka 20, ni Mwekundu wa kweli na sasa
anasomea Beji za Ukocha wa Kulipwa.”
Nae
Mchambuzi wa Sky Sport, Jamie Carragher, amesema Giggs atafaa kwa kazi hiyo
ingawa wanahitaji Kocha mzoefu kama vile Jurgen Klopp wa Borussia Dortmund.
No comments:
Post a Comment