MTOTO
wa miaka saba wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Mkata wilayani
Handeni, Tanga amebakwa na babu yake na kumsababishia maumivu makali na
kumwagika damu nyingi.
Tukio
hilo lilibainika wakati mtoto huyo akiwa darasani na wenzake ambapo alianza
kuvuja damu nyingi hali iliyowafanya wanafunzi wenzake kutoa taarifa kwa
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Moses Kimlayi, aliyefika kushuhudia tukio hilo.
Baada
ya kupewa taarifa hiyo Mwalimu Kimlay alimkabidhi mwanafunzi huyo kwa walimu wa
kike kwa lengo la kumchunguza kama kweli kuna unyama aliofanyiwa. Baada ya
kumhoji mwanafunzi huyo alisema babu yake alimbaka na kumtishia asimueleze mtu
yeyote.
Creit: Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment