![]() |
| Rais wa Shirisho la soka nchini (TFF)Jamali Malinzi (kushoto)alipotembelea Ofisi za Shirikisho la Soka Africa (CAF) kulia ni Rais Mstaafu wa (TFF) Leodigar Tenga na Issa Hayatou (Katikati) |
BAADHI ya Wakazi waliokuwa wamejenga katika eneo ambalo
shirikisho la soka nchini kwa kushirikiana na shirikisho la soka duniani (FIFA)
wanatarajiwa kujenga uwanja wa Kimataifa wamelalamika kuwa serikali bado
haijawalipa fidia ili kuweza kupisha ujenzi wa uwanja huo.
Hatua ya wakazi hao inatokana na kuona Rais wa Shirisho
la soka nchini (TFF)Jamali Malinzi akitembelea uwanja huo na kuanza mikakati ya
ujenzi wa uwanja huo ambao unatarajiwa kugharimu mabilioni ya fedha za
kitanzania.
Wakizungumza katika nyumba zao wanazoishi ndani ya eneo
la shirikisho hilo lililopo Mnyanjani jijini Tanga baadhi ya waathirika hao
ambao wengi wao ni akina mama Christina Lucas alisema wamekuwa wakihangaikia
fidia kila kukicha kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya ili waweze kupisha ujenzi wa
uwanja wa kimataifa bila mafanikio yoyote.
Alieleza zaidi kuwa baadhi yao wameshapewa
maeneo ya kwenda kujenga nyumba baada ya serikali skuridhia ombi lao lakini
fidia ndio imeshindwa kutoka hadi wakati huu kitendo ambacho kinawaweka kwenye
wakati mgumu.
Naye Zabila Iddy alisema wanaiomba serikali kuharakisha
zoezi hilo ili shirikisho la soka la kimataifa Fifa kwa kushirikiana na CAF na
TFF waweze kuanza ujenzi wa uwanja huo haraka iwezekanavyo.
Hata hivyo akizungumzia suala hilo,Mjumbe wa kamati ya
utendaji
TFF,Khalid Mohamed alisema tayari taratibu za kuwalipa zilishafanyika kwa waathirika hivyo watawasiliana na viongozi wa serikali ili kujua zoezi hilo limefikia wapi.
TFF,Khalid Mohamed alisema tayari taratibu za kuwalipa zilishafanyika kwa waathirika hivyo watawasiliana na viongozi wa serikali ili kujua zoezi hilo limefikia wapi.
Jitihada za kumpata mkuu wa wilaya ya Tanga ili kuweza kuelezea
malalamiko hayo ya waathirika ambao wamedai wamekuwa wakifika kwake mara kwa mara bila mafanikio zinaendelea.

No comments:
Post a Comment