![]() |
| VIONGOZI WA YANGA (BIN KLEB KULIA NA KATABARO KUSHOTO)WAKIWA NA OKWI |
|
SHIRIKISHO
la Soka la Kimataifa (FIFA) limemuidhinisha mshambuliaji Mganda, Emmanuel
Arnold Okwi kuchezea klabu ya Yanga ya Dar es Salaam.
Katibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Celestine Mwesigwa ameiambia BIN ZUBEIRY muda huu kwamba, FIFA imewaandikia barua ikiwaambia Okwi ni halali kuchezea Yanga SC.
Januari
22 mwaka huu ikiwa ni siku mbili tu kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya
TFF ilisimamisha usajili wa Mganda huyo Yanga ili kwanza upatikane ufafanuzi
kutoka FIFA juu ya uhalali wake kucheza timu hiyo ya Jangwani akiwa
anatambulika kama mchezaji wa Etoile du Sahel ya Tunisia.
|
Kamati ya
Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF iliyokutana Januari 22, mwaka huu kupitia
masuala mbalimbali, ilisema imesimamisha usajili huo baada ya kubaini kuwa Okwi
aliruhusiwa kuichezea SC Villa ya Uganda kwa kibali maalumu kutoka FIFA.
Okwi
ambaye aliingia kwenye mgogoro na klabu yake ya Etoile du Sahel ya Tunisia
aliruhusiwa na FIFA kuchezea SC Villa kwa kibali maalumu (provisional permit)
cha miezi sita ili kulinda kiwango chake wakati suala lake dhidi ya Etoile du
Sahel likishughulikiwa na shirikisho hilo la kimataifa.
Kulikuwa
kuna kesi tatu FIFA kuhusiana na suala la mchezaji huyo, Okwi ameishitaki klabu
hiyo FIFA kwa kutomlipa mshahara, Etoile du Sahel imemshitaki mchezaji huyo kwa
utoro. Nayo Simba imeishitaki Etoile du Sahel kwa kushindwa kuilipa ada ya
mauzo ya mchezaji huyo ambayo ni dola za Marekani 300,000.
Hivyo, TFF iliiandikia FIFA kutaka kujua iwapo mchezaji huyo anaweza kucheza Ligi nchini Tanzania wakati Etoile du Sahel ikiwa imefungua kesi katika shirikisho hilo la kimataifa ikidai Okwi bado ni mchezaji wake na majibu yamewasili TFF Mganda huyo akihalalishwa kuendelea na kazi Yanga.

No comments:
Post a Comment